Kwanza nianze kwa kuwapongeza kwa uteuzi mliopata na kuwatakia kila
kheri kwa imani hiyo mlopewa na NEC ya chama chetu .
Pili nitumie fursa hii kumpongeza Mwenyekiti kwa kuendesha kikao
ambacho leo kimetuletea PICHA mpya ya vijana na Wazeee katika CC na
Sekretariet ya chama na kuzaliwa upya kwa ccm kwa maana ya HISTORIA
KUANDIKWA kutokana na maamuzi yaliyofikiwa Dodoma.
Ningependa kutumia nafasi hii kuwaambia viongozi wetu sasa ni wakati
wa chama kukabiliana na changamoto zinazotukabili hatua hii, ya sura
mpya haijamaliza bado matatizo yanayotukabili kama chama kinachoongoza
taifa hili,na msirudie makosa yaliyofanyika toka kipindi cha 1995
mpaka leo ya chama kubaki na kufanya siasa za PERSONALITIES na kuacha
siasa za ISSUE na Nguvu nyingi kuzipeleka katika Formular ya Character
assasination ambayo kwa muda mrefu imekiumiza chama na kutufanya
kufika hapa tulipo leo ambapo viongozi wote wachama walichafuka na
kukosa heshima katika PUBLIC jambo ambalo lilitugharimu kwa Muda
Mrefu.
NAPE na JANUARY ni uwakilishi wa vijana katika nafasi nyeti mlizopewa
na mnawakilisha vijana wengi,binafsi nina imani kubwa na nyie bcs sina
shaka juu ya uwezo wenu wa kusimamia mambo magumu hata kama wengine
hawayapendi,changamoto kubwa mlionayo na kuthibitisha matendo yenu
yaendane na vijana wa sasa,mawazo yenu yaendane na vijana wa
sasa,fikra na issues mtakazo simamia zifananne na ziwakilishe asilimia
60 ama 70 ya watu wa nchi hii ambao ni VIJANA,msiishi kama
waliotangulia hatutarajii na nyie kuiendesha CCM kwa mfumo wa NIDHAMU
YA WOGA,ama mfumo wa kiuchaguzi uchaguzi jambo ambalo limekiumiza
chama chetu kwa kiwango kikubwa January IDARA YAKO INAITWA IDARA YA
SIASA NA MAMBO YA NJE alikukabidhi majukumu alijikita mambo ya nje na
kuacha fuction ya siasa.
CC na Sekretariet huu ni wakati wa kuisimamia SEREKALI ili itimize
matarajio ya watanzania wengi,mnawajibu wa kuhakikisha mkataba wetu na
watanzania ambao ni ilani ya uchaguzi inasimamiwa na inatekelezwa
umefika wakati sasa wa chama kuwa kiranja mkuu wa serekali kwani
tuloshinda ni ccm na serekali ni AGENT wa chama kutekeleza yale ambayo
tuliwaahidi watanzania,its a high time muwe na utaratibu wa ku
evaluate serekali na msisite kumshauri RAIS kumwambia hapa waziri
flani hatekelezi wajaibu wake NEC iwe sehemu ya kuevaluate perfomance
ya serekali kila QTR mfumo wa utendaji usiwe wa KI IYENA IYENA the
world has changed na Variables zimebadilika sana,CC lazima iwe THINK
TANK chama na si vikao vya kuchuja wagombea na kupitisha yale ambayo
mwenyekiti anataka ama anashauri,lazima dhana ya kuhoji ichukue nafasi
chama lazima kikemee pale serekali inapokosea msisite kuiambia
serekali hili hapana halikuwa sehemu ya AHADI zetu LAZIMA kila jambo
chama kiwe na uhakika serekali inapotaka kutekeleza imejiandaa
kulitekeleza tusikosee ku hanlde issue kama tulivyokosea ku HANDLE
issue ya katiba, na hapa nipongeze uamuzi wa kufuta HATI ya DHARURA
ktk sheria hii inayohusu mchakato wa katiba.
Chama kina tatizo kubwa la COMMUNICATION STRATEGY we hope JANUARY na
NAPE mtabadili mfumo wetu wa kujibu mambo kwa mzaha na kejeli ma na
mazoea muubadili ili HOJA ZIJIBIWE KWA HOJA, NAPE usirudie wala
kufanya makosa ya kuwatumia watu wasio kuwa na HESHIMA kwenda ktk
PUBLIC kujibu hoja yoyte inayohitaji THINKING, usiruhusu jambo
litakalo haribu heshima ya chama kwa hoja tu MBONA WAO WANATUZOMEA NA
SISI TUKUSANYE WATOTO WAKAZOMEE ,now CCM must act obave diry politics
bcs dhamana ya nchii hii ipo mikononi mwetu si lazima kujibu tusi kwa
tusi.
CC na Sekretariet,mnajukumu la kuibana serekali na kuisimamia
kuhakiksha uchumi unakua,ajira zinapatikana,mfumuko wa bei unatafutiwa
njia za kuudhibiti,mawaziri wanafanya kazi na kutoka
LIKIZO,wanasimamia majukumu yao na kufanya maamuzi magumu bila
kusubiri kila JAMBO mpaka RAIS alitolee majibu,lazima kuwepo
PERFOMANCE APPRISSAL system ambayo chama kitatumia kupima utendaji wa
mawakala wake ambao ni serekali,leo bei ya mafuta imepanda,vyakula
vimepanda,thamani ya shilingi inashuka,maisha yanakuwa magumu kwa
watanzania wengi,sekta ya elimu inachangamoto nyingi za kisera,na
kimfumo,chama kinahitaji WELEDI katika kusimamia serekali na hilo ni
jukumu ambalo lazima mlifanye.
Mnawajibu wa kusimamia PARTY COCUS ili bunge litumike katika ubora
wake na wabunge wetu muwanoe ili kukidhi standards za kusimamia hoja
na ilani ya chama.
Nidhamu hasa kwa watendaji katika ngazi za wilaya na mikoa ni wajibu
wenu kuhakikisha huko chini tatizo la RUSHWA ndani ya mfumo mzima wa
chama linakwisha vijana wengi wanashindwa kukipenda chama chetu kwa
kuwa huko chini kuna MIUNGU WATU,ni lazima CONCEPT ya utumishi ichukue
nafasi ili wenyeviti wetu na makatibu wetu wasiwe wafalme wasimamie
COUNCIOUL ili zitekeleze ilani ya uchaguzi kwani HUO NDIO MKATABA WETU
NA WATANZANIA.
Mwisho niwaombe CCM IMEUMIA SANA KWA POLITICS ZA CHARACTER
ASSASINATION ,POLITICS ZA PERSONALITIES na kuacha kusimamia mambo ya
msingi yanayowaumiza watanzania wengi,RUSHWA,(UFISADI),Tatizo la
UADILIFU,UKOSEFU WA UZALENDO,ni udhaifu wetu wa kutosimamia MAADILI YA
VIONGOZI na hasa tulipofuta AZIMIO LA ARUSHA,hatuna GUIDELINE juu ya
maadili ya VIONGOZI na wanachama,umefika wakati wa chama kulitazama
upya AZIMIO LA ARUSHA ambalo tuliamua kulifuta na kulizika chama
kiamue kulitazama tena kulirudisha pia kufanya mabadiliko pale
tunapoona linahitaji,but MSINGI wa azimio la arusha TUNAUHITAJI TENA.
Mwigulu una mzigo mkubwa wa ku reforme mfumo wetu wa uchumi ndani ya
chama ni wajibu wako kupitia idara yako kuzifanyia audit mali za ccm
ili ktk ngazi za wilaya,mikoa,kata,na mashina tuwe na uwezo wa
kiuchumi kuondokana na tabia ya kutegemea wafadhili na wafanyabiashara
mawilayani na mikoani ili kuwapa uwezo watendaji wetu na viongozi
kufanya maamuzi yanayohusu mustakabali wa chama chetu.
Politics ni uchumi if we are weak economically na sisi kutegemea
RUZUKU CCM tutakuwa na hali mbaya ni wajibu wako kufufua miradi
iliyowahi kufa na kuisimamia kiukamilifu ,tunaviwanja vingi ni wakati
wa kuanzisha Strategic ptnership na mashirika kama NHC na mengine ili
kuwekeza ktk real estate, ALL IN ALL LAZIMA MZEE UPAMBANE . ALL THE
BEST
Niwatakie kila la kheri ktika utekelezaji wenu wa majukumu na mfahamu
kuwa matarajio ya wana ccm ni kubwa sana ninawaombea kwa mungu kila la
kheri MUNGU IBARIKI TANZANIA.MUNGU IBARIKI CC
inShare