Mwanakijiji kushoto akiwa na mwandishi wa habari wa Radio Ebony Fm wakifuta machozi kutokana na mabomu yaliyopigwa na askari hao kuwatawanya wanafunzi hao
Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa wanafunzi zaidi ya 10000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.
Hadi hivi saa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao .
Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo .
Undani wa habari hii ya picha zaidi zitakujia hivi punde katika mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com
chanzo cha habari wanabidiigroup, chanzo halisi www.francisgodwin.blogspot.com
No comments:
Post a Comment