Saturday, August 23, 2014

MAZUNGUMZO YA MARK SCHROEDER NA RAIS KIKWETE




Mark Schroeder: Hello, I'm Mark Schroeder, Vice President of Africa Analysis at Stratfor. I had a recent conversation with the President of Tanzania, Jakaya Kikwete, following his participation at the recent U.S.-Africa Summit that took place in Washington, D.C. President Kikwete describes his vision for Tanzania for the years to come.
---
Mark: You joined us in Texas immediately following the historic United States-Africa Summit, the first time that the United States government has hosted such a summit. Could you describe your observations of the U.S.-Africa Summit that just concluded in Washington?
President Jakaya Kikwete: What I can really say is first, my deepest appreciation to President Barack Obama for conceiving the idea of hosting this summit. We have been exposed or we have had an opportunity to meet the mega players in the U.S. economy. These are companies that have not been easy for African heads of state and government to get access to. And this is really a game-changer, because what is it that we are looking for from Africa? Well it's for promoting investments, promoting trade, we're looking for technology, we are looking for skills, transfers, and this summit has made it possible to create the ambience for the realization of this dream.
Mark: From a political standpoint, the country is a significant role model in the region, in the East African region on the continent and abroad, but the country really models stability. We have seen, unfortunately, conflict in other countries of the region, but could you tell us what are the characteristics of Tanzania that has really modeled stability in that country and really sets that country apart?
President Kikwete: I think it's the pursuit of sound political and economic policies in the sense that politics and economic policies that have been inclusive. Nobody is being discriminated against or being denied the right to access the political or economic because of his ethnicity or because of his tribe, because of his religion or the part of the country that he comes from or because of his gender. I think our first leader really created the foundations for this. He made it clear that if we discriminate each other on the basis of ethnicity, religion, color of the skin or tribe or the area that we come from, we are going to tear apart the country. So, he laid these foundations and fortunately the successive leaders have maintained this policy, have advanced this policy, and it is actually in my view what has really delivered.
Mark: If I could just ask you Mr. President, if you could describe the infrastructure program that you have, once again, that really enables Tanzania to position itself in two regions, the East Africa region, the Southern African region, but as a part of this greater Indian Ocean base as well connected to South Asia, East Asia, it's a really dynamic, large region. Could you describe Tanzania's position there?
President Kikwete: Especially ports, which is a very critical factor for us. The port of Dar es Salaam, we are building two new berths, Berth 13 and 14. We are operating the seven berths, Berth number one through seven, which because we a re looking for support from our development partners but we are also leveraging private sector participation on a PPP basis to develop these ports. Then of course these ports, Tanzania is situated in, the geography of Tanzania is another resource of this kind. We are bordering Uganda, Rwanda, Burundi and the Democratic Republic of the Congo, Zambia, Malawi that have been using the port of Dar es Salaam.
Mark: Yes.
President Kikwete: So we now have to deal with the railways, where the central corridor which links the port of Dar es Salaam with Uganda, Rwanda, Burundi, and the Democratic Republic of the Congo, we're upgrading that one from a narrow gage to a standard gage. Then we are extending the railway line into Rwanda, onward to the Congo, into Burundi and onward again to the Congo. The standards have been completed. It will cost us about $4.1 or 4.2 billion. So there is so much on the infrastructure side that the way we are doing, but why are we doing it? Because we are seeing poor infrastructure impedes growth and development in a big way. We are building 11,000 kilometers of optic fiber, and nationwide optic fiber network. The whole of the eastern side of the African continent is not being connected to the international information highway. There is no optic fiber network submarine linking that. Now South Global has built what we call the SEACOM. It has landed south of Dar es Salaam, but as we are planning to do that we also started working on the nationwide optic fiber network so that when a submarine cable lands in Dar es Salaam we will be able now to make use of it and connect the country to this cable so that we get into the super highway.
Mark: In one advisory study that Stratfor has done, called the Post-China 16, it has really identified Tanzania because of those qualities, because of infrastructure developments, Tanzania has been set apart. The last word to you, Mr. President, is you have intimated the bright future for Tanzania. If you could just conclude with the word of Tanzania in a few years to come, please tell us.
President Kikwete: The other objective is to develop Tanzania into a middle-income country by 2025. By the year 2025, we will have the GDP per capita of $3,000. That's one, but also a highly educated and highly skilled population, we call a knowledge society, a highly knowledge society. Increase the productivity of the country. Make it a country semi-industrialized economy, but competitive enough. Then of course, we are also the fourth to put on, in fact to here, has been also ensure the country is well-governed, good governance, rule of law, human rights and all these vices in society are being fought mercilessly. So these are the four main objectives. It's a tall order, it looks not feasible, but when we started with about $300 GDP per capita, we are now close to $800. So I believe in the remaining ten years we will be able to get there and now of course there is natural gas coming in, coming on stream. It should certainly open up now the opportunities for the growth of the economy. So I'm really saying the future is going to get to a middle-income country by 2025. It's a tall order but I think with the long-term perspective plan we have the road map, we have the benchmarks. I'm optimistic that we can gradually become a middle-income country.
Mark: Thank you President Kikwete that has been a tremendous conversation, and really under your leadership Tanzania has achieved so much already but with the plans that you have initiated that you have just described to us with the resources that are being mobilized from a human capital basis, from an economic development basis, the future for Tanzania is bright. It has been an honor to host you here in Texas at the Stratfor offices. It has been an honor to have you after the historic U.S.-Africa Summit. Thank you again for being on the Stratfor conversations program President Kikwete.
President Kikwete: The pleasure is mine. Thank you. Thank you for having me here. Thank you for the support. We look forward to continued cooperation with Stratfor.
Mark: Thank you sir.




HONGERA BEN SAANANE

Maamuzi Rasmi juu ya barua yangu ya mgogoro wa kikanuni/masharti ya uchaguzi wa baraza la vijana Chadema(BAVICHA) Taifa yamefanyika.
Fomu za uchaguzi zilizotolewa tarehe 12/08/2014 , liliwekwa sharti kuwa mgombea awe na miaka 18-30(Awe amezaliwa 1984 na kuendelea).
Sharti hili lililowekwa kwenye mabano lilinisukuma ku-challenge kanuni/masharti/mahesabu hayo pamoja na masharti mengine kwa kufuata taratibu za chama kama nilivyowaeleza na nikaahidi kusubiri uamuzi
Hoja yangu ilikua kama aliyezaliwa tarehe 01.01.1984 ana haki ya kugombea kwanini isiwe mimi niliyezaliwa tarehe 13/12/1983 yaani wiki mbili na nusu kabla yake kwa kuwa hadi siku ya uchaguzi atakua na miaka 30 na miezi 9 na siku 10 wakati mimi nitakua na miaka 30 na miezi 9 na siku 28 halikadhalika yule aliyezaliwa tarehe 11/09/1983 atakua na miaka 30 na miezi 11 na siku 30 hadi siku ya uchaguzi tarehe 10.09.2014.
Na kwamba ingekua sahihi kama sharti hilo "SHARTI NDANI YA MABANO" lingetamka sawi kuwa mgombea asiwe amefikisha miaka zaidi hadi ifikapo siku ya uchaguzi.Hii ndio ilikua hoja yangu.
Nilirejea katiba na miongozo yetu na kanuni za uchaguzi uliopita wa Baraza la Vijana uliofanyika Mwezi Mei 2011.
Maamuzi ni kuwa wagombea waliozaliwa kuanzia mwaka 1984 ndio watakaokuwa eligible kugombea kama inavyoonekana kwenye fomu zitakazojazwa na wagombea na zipo pia kwenye tovuti ya chama.
Kutokana na maamuzi haya nasikitika kuwatangazia vijana wenzangu kuwa ,kufuatia "SHARTI HILO NDANI YA MABANO " NIMEJIENGUA RASMI KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI KUWANIA NAFASI YA JUU KUONGOZA BARAZA LA VIJANA CHADEMA (BAVICHA).
Maandalizi mliyonishauri niendelee nayo wakati nasubiri uamuzi yatasitishwa
Maandalizi yote ya mkutano na waandishi wa habari kesho Travertine Hotel tumeyasitisha rasmi,Maandalizi ya kurejesha fomu jumatatu ambayo jeshi la polisi liliarifiwa na kukiri kupokea barua iliyoandikwa na vijana waliotaka kunisindikiza kurejesha fomu kuanzia viwanja vya BIAFRA kuelekea Makao makuu yamesitishwa.
Kwa moyo wa kipekee na kwa unyenyekevu mkubwa,nawashukuru marafiki zangu wa karibu na wa mbali,nawashukuru marafiki wa BAVICHA kwa maandalizi kabambe ya kampeni,Nawashukuru ninyi marafiki zangu hapa Facebook na mitandao mingine kwa kuniunga mkono kwa wingi wenu na kujitolea kupambana na dhuluma na hila chafu chafu za watu wachache sana waliokua wakifanya siasa chafu katika safari hii.Mlijitolea kulinda haki,misingi na falsafa ya chama chetu na pia principle zenu kwa kile mnachoamini bila woga.Mlisimama kidete
Ninyi mmekua Nanga yangu initulizayo katika dhoruba.
Ninatambua thamani na mchango wenu kwangu.
Kuna wale walioomba kuchangia kampeni na ziara yangu,ziara ya kufufua ndoto ya mashujaa wetu na kuitaka/kuirudisha Tanzania (Reclaiming Tanzania ).
Sina cha kuwalipa. Nawashukuru sana kwa kusimama nami . Mwenyezi Mungu awajalie kila lililo la kheri nanyi.
Ninafarijika na kuona fahari kuwa chama chetu kimekua sambamba na kasi ya ukuaji wa Teknolojia pengine kuliko chama kingine nchini.
Haikushangaza sana kuona idadi kubwa ya viongozi waliochaguliwa kwenye majimbo na wilaya na hasa tuko nao hapa na kwenye mitandao mingine kama Watsap.
Hakika kampeni za uchaguzi huu tungefanya mageuzi makubwa ya matumizi ya mitandao katika siasa.
Wale wote waliong'ang'ania fikra za ukale(Primitive mentality) tungewaziba midomo.
Mara kadhaa kupitia mitandao hii na ana kwa ana nimekua nikihimiza wale wote wenye nia na dhamira ya kupigania mabadiliko wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi.
Wengi walifanya hivyo na walishinda kwa kishindo na hata chaguzi za mikoa.
Chama chetu kimekua kuliko wakati mwingine wowote.
Chama ni kikubwa kuliko sisi.Tukilinde kama mboni ya jicho .
Kukilinda CHADEMA hata kujitoa sadaka binafsi,ni Sadaka kwa Mageuzi na sadaka hii ni hazina isiyooza kwa vizazi vijavyo vya watanzania.
Mwenyezi Mungu atulinde.
Tusikubali kuingia katika majaribu au mitego yoyote itakayotugawa.Tusikubali kuwa katika upande mbaya wa historia ya harakati za mageuzi.
Safari bado ni mbichi,tutizame tulikotoka na kisha tutazame mbele.Wapo waliofukuzwa /kunyimwa kazi (Mimi ni mmojawapo) ,walioachwa ,waliojeruhiwa na kupata ulemavu na waliopoteza maisha kwa ajili ya CHADEMA na kutafuta haki za kiraia.
Tuendelee kujiimarisha kama taasisi na ni rai yangu kuwa ukomavu wa kisiasa unahitajika zaidi kutokana na ukweli kuwa uchaguzi ndani ya chama ni mgumu kuliko unapopambana na wagombea kutoka nje ya chama.
Ni katika uchaguzi kama huu ,marafiki na mahasimu watajipambanua lakini kitu bora na cha muhimu zaidi mahasimu wanapoonyesha uhasimu katika hoja huwaimarisha wote pamoja na taasisi tofauti na wale wenye siasa za mitaroni.Hao ni kuwapuuza na kusonga mbele.
Tuendelee kuogelea kuelekea kina kirefu zaidi.
Wale wenye hila na nia ovu kama mlivyoshuhudia siku za karibuni,wasisahau kuwa tutaendelea kukutana kwenye kordo za siasa.I'm there to stay.
Sitawafuata kwenye huko vichochoroni kwenye mitaro ya "SIASA MAJITAKA".
Historia kwangu sio gereza,bali ni darasa.Kuna wale waliowahi(labda Walitabiri) na kuandika kwenye mitandao ya kijamii hata kabla fomu hazijatolewa kuwa Mwisho wa Ben Saanane Umefika.Wajitafakari Upya.
Uamuzi huu Sio alama ya Nukta,Bali ni alama ya Mkato Katika Safari yangu ya Kisiasa.Wala sio alama ya Mabano.
Nilipoenguliwa uchaguzi wa BAVICHA mwaka 2011 kwa tuhuma za kuunda Alliance haikua alama ya Nukta katika Safari Yangu.
Nilipoadhibiwa na Baraza la Vijana ambapo mojawapo ya makosa ilikua kutoa tuhuma za usaliti hadharani dhidi ya aliyekuwa naibu katibu Mkuu Zitto Kabwe Tarehe 5 January 2013 na kuzuiwa kugombea nafasi yoyote ndani ya baraza la vijana kwa muda wa mwaka 1 haikua alama ya nukta, bali ilikua alama ya mkato katika safari yangu kisiasa.
Kama nilivyowaahidi ,nitaendelea kukilinda na kukijenga chama chetu na safari hii ya mapambano imezidi kutiwa chachu.
Kuna kisa kimoja cha kifalsafa kwenye Biblia.Kisa cha Mama aliyeiba Mtoto na kesi kupelekwa kwa mfalme Sulemani baada ya utata mkubwa juu ya mams halisi wa mtoto na baina ya wanawake wawili waliokua wanamgombania.Aliamuru Panga liletwe mbele yake kisha mtoto akatwe ili wagawane sawa.Mwanamke Mmojawapo akaridhia haraka wakati mwingine alijibu 'Ewe Mfalme,Ni bora akabidhiwe huyu mwenzangu ' Busara zikamtuma Sulemani kuwa Mama halisi ni yule mwenye uchungu na mtoto.Tusiruhusu sasa kuingia upande mbovu.
Nimepokea Ushauri mwingi kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki .Msiumie kwa uamuzi huu,tuuheshimu .
Tutaendelea kuwaabisha wale wote wa nje wanaotazama uchaguzi wetu wa ndani kwa jicho la husuda.Maadui wa demokrasia na haki tutawashinda kwa ukomavu wetu wa kisiasa tu.
Kaka yangu Godbless Lema na baadhi ya wabunge vijana na madiwani wetu, nimeheshimu Ushauri wenu.Dada yangu Halima Mdee nimeendelea na nitaendelea kuheshimu ushauri wako.
Nina maamuzi mengine nitakayochukua baada ya kutafakari kwa kina ndani ya saa 48 zijazo.
Mwanamapinduzi Ninayemuhusudu sana Rais wa Zamani wa Venezuela Hugo Chavez alishawishi na ameendelea kunichochea kwa kauli yake kwenye nukuu siku siku zote "There is no turning Back".
Mwenyezi Mungu awabariki nyote.
Aluta Continua ,Victory Ascerta....


CHANZO MTANDAO WA WANABIDII.

Wednesday, August 6, 2014

SALAMU ZA ACT- Tanzania

SOTE NI WATANZANIA

Ndugu Viongozi wa vyama vya siasa nchini, wanachama wa vyama mbali mbali vya siasa nchini, wadau mbali mbali wa siasa nchini na watanzania wote kwa ujumla; tunapenda kuwasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!

Chama cha ACT-Tanzania kinapenda kuwapa salamu hizi kufuatia wasi wasi ambao umekuwa ukioneshwa na baadi ya Viongozi wa vyama vya siasa, wanachama wao na hata washabiki wao juu ya ujio wa Chama kipya cha ACT-Tanzania.Kumekuwa na wimbi la baadhi ya watu kutoka vyama kadhaa vya kiaisa kulalamika kwamba eti chama cha ACT-Tanzania kimekuja kuwamaliza kisiasa.

Chama cha ACT-Tanzania kinapenda kutuma salamu kwa vyama vyote vya siasa nchini na wanachama wao kwamba; Chama cha ACT-Tanzania hakijaja Kuvimaliza vyama vyao wala kupambana na mtu yeyote wala chama chochote cha siasa nchini, bali kimekuja kupambana na matatizo sugu yanayomkabili mtanzania kupitia misingi, falsafa na itikadi zake.ACT-Tanzania imeanzishwa katika misingi yake yenyewe, Inajijenga katika misingi yake yenyewe,Itajiimarisha katika misingi yake yenyewe, Itatembea katika misingi yake yenyewe, Itasimama katika misingi yake yenyewe na kama ni kuanguka; basi itaanguka kwa kutokusimamia misingi yake yenyewe.Uwepo wa ACT-Tanzania hautegemei wala hautatagemea uwepo wa vyama vingine au operesheni za vyama vingine.Kwa lugha nyingine ni kwamba uwepo wa ACT-Tanzania hautategemea matukio bali misingi yake yenyewe.

Hata hivyo, kwa kuwa lengo kuu la ACT-Tanzania ni kupambana na matatizo sugu yanayomkabili mtanzania ambayo bado yanasumbua sana na kuleta machungu katika maisha ya watu, ili kuleta unafuu na furaha katika maisha ya mtanzania; lengo hili litafikiwa kwa ukamilifu wake kwa chama kupewa mamlaka ya kuiongoza nchi.Mamlaka hayo yatatoka kwa wananchi watakaoikubali misingi itikadi na falsafa za chama.Kwa kuwa katika uchaguzi chama kinachoshinda ni kimoja, ni wazi kwamba ACT-Tanzania itakaposhinda; vyama vingine vyote vitabaki kuwa vyama vya upinzani wakati ACT-Tanzania ikisimamia itikadi yake na ikitekeleza sera zake lakini hii haimaanishi kwamba ACT-Tanzania imekuja kuvipoteza vyama hivyo katika sura ya siasa za Tanzania! kwani hilo sio lengo la msingi la ACT-Tanzania.

Kadhalika tunafahamu kwamba kutokana na ubora wa falsafa, misingi na itikadi za ACT-Tanzania, Uwajibikaji,uwazi na uadilifu wa viongozi wa chama tulionao na tutakaokuwa nao, wanachama wengi kutoka vyama vyote nchini, watakuwa wakijiunga na ACT-Tanzania makundi kwa makundi.Hata hivyo hiyo haitakuwa inamaanisha kwamba tuna uadui na vyama wanakotoka wanachama hao.Tutafanya nini sasa! katika hali hiyo ndipo tunaposisitiza kwamba itatupasa tuwe na uvumilivu wa kisiasa.Tunawashauri wale watakaoona kwamba chama chetu kinafanya vizuri, wasitujengee uadui bali watuunge mkono au watuvumilie tu.

Kuhusu watu wanaotumia mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kudai kwamba wao ni wana ACT-Tanzania, na chama hiki kimekuja kupambana na watu fulani fulani, nao wanasema kwa niaba ya chama! na watu wanaotunga habari na kudai zimesemwa na viongozi wakuu wa chama kwamba ACT-Tanzania imekuja kwa lengo kuu la kuua vyama vya watu fulani,Tunawaomba watanzania muwasamehe kwani kuna siku watajua kwamba wanachokifanya si sahihi na wakarudi kwenye njia ya ukweli na ustaarabu.

Mwisho, ACT-Tanzania kupitia Ofisi yake ya Mawasiliano na Uenezi, Inajenga na itaendelea kuimarisha mahusiano na vyama vyote nchini kwa kadiri itakavyowezekana kwani chama kinaamini kwamba sote ni watanzania na zaidi ya hapo sote ni watu.Chama kinakaribisha na kinapokea ushauri wowote kutoka kwa yeyote bila kujali chama chake, kitaupitia na kuuchambua na kila itakapoonekana unafaa, utafanyiwa kazi.Chama kiko tayari kushirikiana na yeyote anayependa ushirikiano katika mambo mema na yenye tija kwa taifa.ACT- Tanzania bado ndio chama kidogo zaidi nchini, hivyo badala ya kukiogopa; ni bora kukishika mkono ili kuimarisha demokrasia.Kadhaalilika Chama kupitia Ofisi ya Mawasiliano na uenezi, kitajenga na kuimarisha uhusiano na vyama mbali mbali duniani hasa vile vyenye muelekeo wa "Mrengo wa Kati Kushoto".

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa la leo na kesho.

ACT- Tanzania ..............Taifa kwanza!,

Mabadiliko na uwazi...........Chukjua hatua!


Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uenezi ya Dar es Salaam leo tarehe 05/06/2014.