JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA MUSTAFA HAIDI
MKULO (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA
SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA
MWAKA 2011/2012
UTANGULIZI:
2
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na
matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Pamoja
na hotuba hii, vipo vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina takwimu
mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinahusu makisio ya
mapato. Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya
kawaida kwa Wizara na Idara zinazojitegemea ambapo cha Tatu
kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa na cha Nne kinaelezea makadirio
ya matumizi ya maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea,
Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo
Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2011 ambao ni sehemu
ya Bajeti hii.
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumpongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa tena kuongoza kwa muhula wa
3
pili wa Serikali ya Awamu ya Nne. Aidha, ninamshukuru sana
Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa
kunichagua kwa mara nyingine tena kuongoza Wizara kubwa na
nyeti, ninamuahidi kuwa sitamuangusha. Pia ninampongeza
Dkt. Mohammed Gharib Billal kwa kuchaguliwa kuwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vile vile,
ninampongeza Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb.) kwa
kuchaguliwa kuwa Mbunge na kuteuliwa tena na hatimaye
kupitishwa na Waheshimiwa Wabunge kuwa Waziri Mkuu kwa
muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Nne.
3. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi Mhe.
Spika Anne Makinda (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Spika na hivyo
kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Bunge katika Afrika
Mashariki. Kuchaguliwa kwako kunatokana na imani kubwa
waliyonayo Waheshimiwa Wabunge kwa kuzingatia busara zako,
uwezo na uzoefu wako ndani ya Bunge hili. Napenda pia
4
kumpongeza Mhe. Job Ndugai (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa
Naibu Spika. Nawapongeza pia mawaziri wenzangu wote pamoja
na Naibu mawaziri wote, kwa kuteuliwa kwao na Mhe. Rais
kushika nyadhifa hizo. Aidha, napenda niwapongeze wabunge
wote kwa kuchaguliwa na kuteuliwa kuingia katika Bunge hili.
4. Mheshimiwa Spika, naomba pia nichukue fursa hii kutoa
shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna
moja au nyingine kufanikisha matayarisho ya Bajeti hii.
Maandalizi ya Bajeti ya Serikali yanahusisha wadau na vyombo
mbalimbali. Kipekee ninaishukuru Kamati ya Fedha na Uchumi
chini ya uenyekiti wa Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda, Mbunge
wa Handeni, pamoja na kamati nyingine za kisekta kwa ushauri
mzuri waliotoa wakati wakichambua mapendekezo ya Bajeti hii.
5. Mheshimiwa Spika, naomba niishukuru kwa namna ya
pekee Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutayarisha
5
kwa wakati Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2011 na
nyaraka mbalimbali za sheria ambazo ni sehemu ya bajeti hii.
Kwa upande wa Wizara ya Fedha, nawashukuru Naibu Mawaziri,
Mhe. Gregory Teu (Mb) na Mhe. Pereira Ame Silima (Mb).
Namshukuru Katibu Mkuu Ndugu Ramadhani M. Khijjah na Naibu
Makatibu Wakuu, Ndugu Laston T. Msongole, Dkt. Servacius B.
Likwelile na Ndugu Elizabeth Nyambibo. Napenda kuwashukuru
Prof. Benno Ndulu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Ndugu
Harry Kitilya, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
na Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya
Taifa. Aidha, napenda kuwashukuru Wakuu wa Idara na
wafanyakazi wote wa Wizara ya Fedha. Vile vile, namshukuru
Mpigachapa Mkuu wa Serikali kwa kuchapisha Hotuba hii kwa
wakati. Mwisho, nawashukuru wataalamu na wale wote waliotoa
mapendekezo kuhusu sera, mikakati na masuala mbalimbali ya
kodi ambayo yamezingatiwa katika kuandaa Bajeti hii.
6
6. Mheshimiwa Spika, huu ni mkutano wa kwanza wa
Bajeti kwa Bunge hili baada ya uchaguzi mkuu wa Rais na
Wabunge uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2010 na kukirejesha
Chama Cha Mapinduzi pamoja na Serikali yake katika kipindi cha
pili cha Awamu ya Nne. Wananchi wana matumaini makubwa
kwa Bunge hili kwamba litasaidia kuongeza kasi ya kuwapatia
maendeleo na kuondokana na umasikini wa kipato unaowakabili
wananchi walio wengi. Hili linajidhihirisha kwa uwepo wa
Waheshimiwa Wabunge wenye umri, jinsia, elimu, na uzoefu
mbalimbali. Ni matumaini ya Serikali kuwa uwepo huo wa
Waheshimiwa Wabunge utakuwa ni chachu katika kuwaletea
maendeleo wananchi kwa ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi.
7. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka wa fedha
unaoishia 2010/2011, imeendelea kutumika kama chombo
muhimu katika kutekeleza Sera na Malengo ya Uchumi na
7
Maendeleo ya Jamii. Katika kipindi hiki, yamekuwepo mafanikio
ya kuridhisha katika kutoa huduma bora kwa wananchi na
kuimarisha miundombinu ili kuwezesha kukua kwa uchumi na
kupunguza umaskini.
8. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2011/12 itazingatia
vipaumbele vifuatavyo:
i) Umeme;
ii) Maji;
iii) Miundombinu ya usafiri na usafirishaji (reli, bandari,
barabara, viwanja vya ndege, Mkongo wa Taifa);
iv) Kilimo na umwagiliaji; na
v) Kupanua ajira kwa sekta binafsi na ya umma.
Bajeti itahakikisha pia kuwa mafanikio yaliyopatikana katika
sekta za elimu na afya yanalindwa pamoja na kuimarisha ubora
wa huduma zinazotolewa.
8
Mikakati ya Kupunguza Makali ya Maisha kwa
Mwananchi
9. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto
zinazowakabili wananchi katika kupambana na makali ya maisha.
Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, pamoja na mambo
mengine, inalenga katika kuchukua hatua za kurekebisha hali
hiyo. Kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji
hatua za makusudi kuchukuliwa na wadau mbalimbali ikiwemo
Serikali, sekta binafsi na mwananchi mmoja mmoja ili kupunguza
makali ya maisha kwa mwananchi. Hatua zitachukuliwa maeneo
yafuatazo:-:
i) Kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma: Kasi
ya ongezeko la bei za bidhaa na huduma nchini pamoja na
mambo mengine inasababishwa na: kuongezeka kwa bei za
9
mafuta katika soko la dunia; kutopatikana kwa umeme wa
uhakika na hivyo kuathiri uzalishaji; na upungufu wa
chakula nchini na nchi jirani. Serikali itachukua hatua
mbalimbali kukabiliana na hali hiyo kama ifuatavyo:
a) Ongezeko la bei za mafuta ya petroli: Ongezeko la
bei za mafuta ya petroli linatokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa bei katika soko la
dunia. Kwa mfano baada ya msukosuko wa uchumi
duniani bei ya mafuta ilishuka hadi Dola za Kimarekani
40 kwa pipa. Kwa sasa bei ya mafuta katika soko la
dunia imefikia takribani Dola 120 kwa pipa ambayo ni
mara tatu ya bei iliyokuwepo awali. Aidha, ongezeko la
bei linachangiwa pia na kuongezeka kwa gharama za
bima ya mizigo kwa meli zinazoleta mizigo nchini
kutokana na tishio la maharamia baharini, uagizaji wa
mafuta wa kampuni moja moja na migogoro ya kisiasa
10
katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa bara
la Afrika. Pamoja na sababu zilizotajwa, bidhaa ya
mafuta ya petroli inapoingia hapa nchini hutozwa
ushuru wa bidhaa (excise duty) na ushuru wa mafuta
(fuel levy). Zipo pia tozo mbalimbali zinazotozwa na
Mamlaka zinazotoa huduma katika mfumo wa uagizaji
na upokeaji wa mafuta. Taasisi zinazotoza tozo hizo ni
pamoja na EWURA, SUMATRA, Shirika la Viwango la
Taifa (TBS), Kiwanda cha TIPER, Mamlaka ya Mapato
Tanzania, Mamlaka ya Bandari na makampuni
yanayoagiza mafuta. Pamoja na hatua zilizochukuliwa
na Serikali za kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na
kuweka viwango maalum vya ushuru wa bidhaa kwenye
mafuta, bado bei ya mafuta imeendelea kuwa kubwa na
kuongeza gharama za maisha.
11
Mheshimiwa Spika, ili kupunguza makali ya ongezeko la
bei ya mafuta nchini, Serikali imeamua kufanya mapitio ya
namna ya kukokotoa tozo zinazotozwa na Mamlaka mbalimbali
kwa lengo la kuzipunguza na zoezi hili litakamilika katika mwaka
wa fedha 2011/12. Aidha, Serikali pia inakamilisha taratibu za
ununuzi wa mafuta kwa wingi kwa lengo la kuyauzia makampuni
ya usambazaji kwa bei ya jumla. Kanuni zitakazotoa mwongozo
katika uagizaji mafuta kwa pamoja zimekamilika na utaratibu
huu unategemewa kuanza katika mwaka wa fedha 2011/12.
Utaratibu huu unatarajiwa kupunguza bei na gharama za
usafirishaji wa mafuta hayo. Pamoja na juhudi hizi za Serikali,
sekta binafsi inahimizwa kuwezesha upatikanaji wa huduma ya
kutumia gesi kama nishati mbadala wa mafuta ya petroli hasa
mijini. Ni matarajio yangu kwamba hatua hizi zitaleta unafuu wa
bei ya mafuta hapa nchini na hivyo kupunguza gharama za
maisha kwa wananchi na kuboresha uchumi kwa ujumla.
12
b) Upungufu wa Nishati ya umeme: Nchi yetu
inakabiliwa na upungufu wa nishati ya umeme kutokana
na kiwango kidogo cha uzalishaji usioendana na
mahitaji. Kwa kuzingatia kuwa umeme una umuhimu
wa kipekee katika kukuza uchumi wa nchi, Serikali
itachukua hatua kadhaa za kukabiliana na upungufu
huu, ikiwemo kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme
wa megawati 100 Dar es Salaam na ule wa megawati
60 Mwanza; kuiwezesha TANESCO kupata mikopo
kutoka taasisi za fedha za kimataifa kwa ajili ya
kununulia mitambo ya uzalishaji na kuangalia upya
namna ya kugawanya shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji
na Usambazaji; kwa lengo la kuiachia TANESCO kujikita
kwenye eneo ambalo ina uwezo nalo kiushindani na
hivyo kuleta ufanisi katika sekta nzima ya umeme.
Aidha, kutokana na kukamilishwa kwa sera, sheria na
kanuni za ubia kati ya Serikali na sekta binafsi (PPP),
13
Serikali itaandaa utaratibu wa kuhusisha sekta binafsi
katika sekta ya umeme na inatarajiwa kwamba baadhi
ya miradi ya uzalishaji umeme itatekelezwa kwa njia ya
ubia kati ya Serikali na sekta binafsi. Serikali
imeshaanza majadiliano na wawekezaji katika uzalishaji
wa umeme kwa ubia katika miradi ifuatayo; Mtwara MW
300, Mpanga MW 144, na miradi ya usafirishaji umeme
wa kV 400 ya Morogoro-Tanga-Kilimanjaro-Arusha km
682 na upanuzi wa Gridi ya Kaskazini Magharibi kwa
mikoa ya Kagera, Kigoma na Rukwa - km 1000. Serikali
inawashauri wananchi kuanza kutumia vyanzo mbadala
vya umeme wa jua, upepo na nishati inayotokana na
biogesi pamoja na kutumia kwa uangalifu nishati ya
umeme iliyopo.
14
c) Kuimarisha Hifadhi ya Chakula: Kutokana na
kuendelea kuwepo kwa upungufu wa chakula
kulikosababishwa na ukame katika baadhi ya maeneo
ya nchi, Serikali itaendelea kuimarisha hifadhi ya
chakula kwa kuongeza ununuzi wa mazao ya chakula
katika Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Serikali (NFRA).
Aidha, hifadhi hiyo itatumika kupunguza bei ya chakula
nchini kwa kusambaza nafaka kwa bei nafuu katika
masoko wakati wa uhaba. Kadhalika, wananchi
wanashauriwa kuendelea kulima mazao yanayohimili
ukame pamoja na kilimo cha umwagiliaji na kuzingatia
kuweka akiba ya chakula cha kutosha.
ii) Kuongeza Ajira: Mheshimiwa Spika, Ukosefu wa ajira,
hasa kwa vijana umeendelea kuwa ni changamoto kubwa,
15
hivyo, Serikali inafanya juhudi za makusudi kupanua ajira
katika maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:-
a) Mpango wa Ukanda wa Kilimo wa Kusini mwa Tanzania
(Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania-
SAGCOT). Mpango huu ni mkakati wa kuleta mapinduzi
ya kilimo ambao utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya
Serikali na na wadau mbalimbali wa kilimo, wakiwemo
washirika wa maendeleo. Utekelezaji wa Mpango huu
ambao ni sehemu ya Kilimo Kwanza, utasaidia
kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi
wanaoishi vijijini kwa kuwaongezea mavuno ya mazao
yao na kukuza ajira miongoni mwa Watanzania. Katika
mwaka 2011/12 Benki ya Dunia inatarajia kuchangia
Dola za Kimarekani milioni 60 sawa na shilingi bilioni
92.8. Tunakamilisha taratibu za kupata fedha hizo na
16
tutawasilisha Bungeni kwa ajili ya kuidhinisha matumizi
yake.
Mheshimiwa Spika, Serikali pia itaendelea kufanya
maboresho ya kilimo cha mazao, ufugaji na uvuvi. Kwa upande
wa mazao, Tanzania ina mabonde mazuri yenye rutuba kwa
kilimo cha mpunga katika mikoa ya Tabora, Mwanza, Shinyanga,
Kigoma, Pwani, Mbeya, Kilimanjaro, Tanga na Morogoro. Chini
ya utaratibu huu, wakulima wadogo wadogo watawezeshwa
kupata huduma za mikopo, ugani, mbegu bora na mbolea.
Utafiti unaonesha kuwa kwa kutumia vizuri mabonde hayo,
pembejeo na tija katika uzalishaji, inawezekana kutoa fursa za
ajira mchanganyiko.
b) Viwanda vya kusindika mazao ya kilimo vitasaidia
kuongeza thamani ya mazao na ajira. Aidha, eneo
jingine la kuongeza ajira ni kupitia mwingiliano (linkage)
17
baina ya viwanda vya nguo na sekta ya kilimo. Juhudi
zinazoendelea za kuimarisha upatikanaji wa nishati ya
umeme kwa kutumia vyanzo mbadala vya umeme wa
maji na mafuta ambavyo ni upepo, jua na biogesi,
zitasaidia kufanikisha mpango wa uzalishaji wa bidhaa
viwandani. Kadhalika, Serikali itaboresha mazingira ya
sekta ya viwanda (vikubwa, vidogo na vya kati), ili
kuviwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
c) Kuongeza kasi ya utekelezaji wa MKURABITA, ili
mpango huu uweze kuchangia ongezeko la ajira.
Serikali kwa kushirikiana na AZAKI, AZISE na wadau
wengine, itaendelea kuwawezesha wajasiriamali
wadogo na wa kati (SMEs), ili kuongeza ajira. SIDO,
VETA na vyuo vya maendeleo ya wananchi na vijana
vitaboreshwa zaidi ili visaidie kutoa mafunzo ya
18
ujasiriamali ambayo yataongeza ajira. Serikali imeweka
utaratibu mzuri wa kuwawezesha waombaji wa mikopo
kwa kutumia dhamana ya Serikali kupitia mifuko iliyo
chini ya Benki Kuu na kupitia benki zao za biashara
kupata mikopo kwa ajili ya shughuli zao za uzalishaji.
Utaratibu huu umenufaisha wajasiriamali wengi ikiwa ni
pamoja na vyama vya ushirika na sekta binafsi.
d) Kuharakisha maboresho yanayoendelea katika sekta ya
fedha na utekelezaji wa sera ya uwezeshaji ambazo
zitasaidia upatikanaji wa mikopo kwa wananchi ili
waweze kupata mitaji na kujiajiri. Hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika eneo hili ni pamoja
na kuharakisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa,
kuanzishwa kwa taasisi ya kuratibu taarifa sahihi za
waombaji wa mikopo (credit reference bureau ) ambayo
itakuwa inahifadhi taarifa sahihi za wakopaji (credit
19
reference databank); na mwisho, kuhamasisha
mashirika ya umma, sekta binafsi na mifuko ya hifadhi
ya jamii kuongeza fursa za ajira katika maeneo yao kwa
kuwekeza katika vitega uchumi na kutoa mafunzo ya
kujiajiri kwa vijana wasio na ajira.
10. Mheshimiwa Spika, ni matarajio yangu kwamba hatua
hizi zitasaidia kuleta unafuu na hivyo kupunguza gharama za
maisha kwa wananchi na kuboresha uchumi kwa ujumla. Serikali
inaomba ushirikiano wa kila mmoja wetu ili hatua hizo zilete
matokeo yanayotarajiwa.
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA SERA ZA BAJETI YA
MWAKA 2010/11:
20
11. Mheshimiwa Spika, Mfumo wa Bajeti wa mwaka 2010/11
ulizingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025; Mkakati wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II); Malengo ya
Maendeleo ya Milenia (MDGs); Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu
ya Mwaka 2005; Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania
(MPAMITA); na Mkakati wa Taifa wa Madeni.
12. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/11,
Serikali imeendelea kutekeleza majukumu yake kulingana na
misingi ya sera ilizojiwekea. Sera hizo zililenga katika kuimarisha
ukusanyaji wa mapato, kusimamia matumizi ya fedha za umma
na uwajibikaji. Aidha, Serikali ilikusudia kuendelea kudhibiti Deni
la Taifa pamoja na kuboresha mahusiano yetu na wahisani
wanaosaidia Bajeti ya Serikali.
21
13. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi jumla
pamoja na misingi na sera za Bajeti, katika kipindi cha mwaka
2010/11, Serikali ilikadiria kukusanya mapato na kutumia kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo jumla ya shilingi
trilioni 11.6. Kwa mwaka huo, Serikali ilipanga kukusanya
mapato ya ndani ya shilingi trilioni 6.0; mapato kutoka Serikali za
mitaa kiasi cha shilingi bilioni 172.6; misaada na mikopo ya
kibajeti shilingi bilioni 821.6; misaada na mikopo ya miradi ya
maendeleo na ya kisekta kiasi cha shilingi trilioni 2.5; mikopo ya
ndani na nje shilingi trilioni 1.3; mikopo ya kulipia dhamana na
hatifungani shilingi bilioni 797.6; na mapato kutokana na
ubinafsishaji shilingi bilioni 30.0.
14. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa bajeti ya
mwaka 2010/11, mafanikio yaliyojitokeza ni pamoja na
yafuatayo:
22
i) Kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani hadi mwezi
Machi 2011 kiliongezeka kwa asilimia 21 ikilinganishwa
na mapato yaliyokusanywa kipindi kama hicho mwaka
2009/10. Aidha, katika kipindi hicho, ukusanyaji wa
mapato uliongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni
390 kwa mwezi mwaka 2009/10 hadi shilingi bilioni 473
mwaka 2010/11;
ii) Kugharamia Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba
2010 kama ilivyopangwa;
iii) Kufanikisha ununuzi wa tani 182,000 za chakula cha
Hifadhi ya Taifa, kwa kutumia jumla ya shilingi bilioni 57,
ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula lililojitokeza
katika baadhi ya maeneo nchini;
23
iv) Kugharamia mafunzo kwa wanafunzi 4,598 katika fani ya
maafisa ugani wa kilimo na mifugo;
v) Serikali imeendelea kulipa madeni ya watumishi
kulingana na uhakiki uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali;
vi) Mishahara na stahili za watumishi ziliendelea kulipwa kwa
wakati;
vii) Serikali imelipa kiasi cha shilingi bilioni 200 kama sehemu
ya gharama kwa ajili ya ununuzi wa genereta zenye
uwezo wa kufua umeme wa megawati 60 kwa mkoa wa
Mwanza na megawati 100 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha, Serikali imechukua hatua za dharura za
kupunguza makali ya mgao wa umeme katika gridi ya
24
Taifa kwa kugharamia ununuzi wa mafuta ya kuendesha
mitambo ya kufua umeme ya IPTL, ambapo jumla ya
shilingi bilioni 18.5 zimetumika;
viii) Kwa ushirikiano na Serikali ya China, Serikali iliendelea
na ujenzi wa jengo maalum kwa ajili ya matibabu ya
moyo katika hospitali ya Muhimbili pamoja na wodi za
kulaza wagonjwa wa saratani katika hospitali ya Ocean
Road;
ix) Kuongeza mtaji kwa shilingi bilioni 50 katika benki ya
rasilimali (TIB) na hivyo kukuza mtaji hadi shilingi bilioni
92. Aidha, shilingi bilioni 20 ziliongezwa kwenye dirisha la
kilimo na kufanya dirisha hilo kuwa na shilingi bilioni 42;
na
25
x) Kufanikisha utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa
wanafunzi 96,328 ambapo jumla ya shilingi bilioni 185
zimetumika, ikilinganishwa na wanafunzi 72,035 na
shilingi bilioni 145 zilizotumika kwa kipindi kama hicho
mwaka 2009/10.
MAPATO YA NDANI:
15. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha
2010/11, Serikali ilitarajia kukusanya mapato ya ndani ya kiasi
cha shilingi bilioni 6,003.6 sawa na asilimia 17.3 ya Pato la Taifa.
Ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, hatua mbalimbali
zilizochukuliwa ni pamoja na:
i) Kuendelea kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato
kwa kuhakikisha kuwa pale inapowezekana malipo
yanafanyika kupitia kwenye mabenki;
26
ii) Kuweka mkakati wa kuboresha huduma za utalii kwa
kutathmini hoteli ili ziwe katika viwango vinavyokubalika
kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato yanayotokana
na ada;
iii) Kuhimiza utekelezaji wa Sheria ya Fedha Na. 13 ya
mwaka 2008 na Waraka wa Hazina Na. 8 wa mwaka
2008/09 inayoelekeza mashirika na taasisi kuchangia
katika Mfuko Mkuu wa Serikali;
iv) Kuendelea kupanua wigo wa kodi kwa kusajili walipa
kodi wapya na kuimarisha uchumi tulivu pamoja na
kuweka mazingira bora ya biashara ili kuwezesha kukua
kwa sekta binafsi;
27
v) Kuendelea kusimamia kwa karibu mageuzi makubwa
yanayoendelea ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,
chini ya mpango wake wa Tatu wa Maboresho wa
Miaka Mitano ambayo yamekuwa msingi wa kukua kwa
ukusanyaji wa mapato ya ndani mwaka hadi mwaka;
vi) Kuchukua hatua za kuboresha ukusanyaji wa mapato
yasiyo ya kodi kutoka Wizara na Idara za Serikali;
vii) Kupitia upya utaratibu wa kutoa misamaha ya kodi kwa
lengo la kuongeza udhibiti; na
viii) Kuendelea kuhakikisha kwamba watendaji wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa wanajengewa uwezo kwa kuwapatia
utaalam wa kutosha ili kuongeza ufanisi katika ukadiriaji
na ukusanyaji wa mapato katika Serikali za Mitaa.
28
16. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2010/11,
Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani, SURA 148. Marekebisho mengi yaliyofanyika katika
Sheria hii yalilenga kutoa kipaumbele katika kukuza uzalishaji
kwenye sekta ya kilimo na mifugo na kuongeza mchango wake
kwenye Pato la Taifa. Hivyo, marekebisho hayo yalijumuisha
kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa mashine na vifaa
vya kukusanyia, kusafirishia na kusindika maziwa pamoja na
vifungashio vya maziwa ili kuhamasisha uwekezaji katika sekta
ndogo ya maziwa na hivyo kuboresha kipato cha wananchi.
17. Mheshimiwa Spika, Serikali ilisamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye mashudu kwa ajili ya chakula cha mifugo ili
kuhamasisha ufugaji bora na kuwawezesha wakulima wa mbegu
za mafuta kupata bei yenye tija kwa mauzo ya bidhaa hiyo;
kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye zana za kilimo,
na huduma za kuzalisha mifugo kwa njia ya kupandisha mifugo
29
na kutumia mashine maalum za kuzalishia/kutotolea vifaranga
pamoja na vifungashio vya juisi za matunda. Aidha, Serikali ilitoa
unafuu maalum wa kodi ya ongezeko la thamani kwenye
mabanda yanayotumika katika kilimo cha maua na kusamehe
kodi ya usafirishaji wa maua kwa ndege kwenda nje ya nchi.
Hatua hizi zimepelekea kuongezeka kwa uzalishaji na usindikaji
wa maziwa, uagizaji wa matanki ya kuhifadhia maziwa,
upatikanaji wa zana za kilimo, pamoja na uzalishaji wa mifugo
na mazao ya kilimo kwa baadhi ya maeneo nchini.
18. Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa unafuu maalum wa kodi
ya ongezeko la thamani kwenye uuzaji wa bidhaa na huduma
zitolewazo kwa wakulima waliosajiliwa au mashamba ya vyama
vya ushirika kwa ajili ya kujenga miundombinu ya mashamba
kama vile mifereji ya umwagiliaji, barabara za mashambani,
ujenzi wa maghala au huduma nyinginezo za namna hiyo; na
kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango cha asilimia
30
sifuri kwenye usindikaji wa mafuta ya kula kwa wazalishaji wa
mafuta ya kula wanaotumia mbegu za mafuta zinazozalishwa
hapa nchini. Hatua hizi kwa pamoja zimesaidia kupunguza
gharama za uzalishaji na kuboresha thamani ya bidhaa.
19. Mheshimiwa Spika, hatua hizi zimepelekea kuongezeka
kwa upatikanaji wa zana za kilimo, pamoja na uzalishaji wa
mifugo na mazao ya kilimo kwa baadhi ya maeneo nchini.
Takwimu za awali zinaonesha kuwa uzalishaji wa alizeti
unatarajiwa kuongezeka kutoka tani 328,533 mwaka 2009/10,
hadi tani 666,030 mwaka 2010/11; uzalishaji wa karanga kutoka
475,918 mwaka 2009/10, hadi kufikia tani 600,300 mwaka
2010/11; na ufuta kutoka tani 146,919 mwaka 2009/10, hadi
kufikia tani 326,660 mwaka 2010/11. Hadi kufikia Aprili 2011,
uagizaji wa vifaa vinavyotumika kuunganisha mabanda maalum
yanayotumika kuzalishia maua (green houses) uliongezeka
kutoka nyumba zenye uzito wa kilo 4,542,959 mwaka 2009/10,
31
hadi kilo 7,181,228. Hata hivyo, matokeo ya hatua nyingine
zilizochukuliwa katika kuboresha uzalishaji kwenye kilimo
yatajitokeza katika muda wa kati na mrefu.
20. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2010/11,
Serikali pia ilifanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato,
SURA 332 kwa kuweka wigo wa ukomo wa maeneo ya
uchimbaji wa madini kwa nia ya kudhibiti gharama zinazotakiwa
kutolewa katika kukokotoa faida itakayotozwa kodi ya mapato
kuwa ni zile zinazohusika; kupunguza kiwango cha chini cha Kodi
ya Mapato yanayotokana na ajira kutoka asilimia 15 hadi asilimia
14, ili kuwaongezea kipato na kuwapunguzia mzigo wa kodi
watumishi wenye kipato cha chini; na kuwataka
wafanyabiashara wenye namba za utambulisho wa mlipa kodi
(TIN), kuzuia asilimia 2 kila wanapofanya malipo kwa wasiokuwa
na namba hizo, kutokana na bidhaa au huduma walizopata
32
kutoka kwao, ili kuwahamasisha wasiokuwa na namba kwenda
kusajiliwa.
21. Mheshimiwa Spika, hatua hii, pamoja na juhudi
nyinginezo ziliwezesha kuongeza idadi ya walipa kodi wapya
ambapo hadi Machi, 2011 jumla ya walipakodi waliosajiliwa na
TIN wamefikia 686,098, ikilinganishwa na lengo la kusajili
walipa kodi 674,442 ifikapo Juni, 2011. Maboresho ya kodi ya
mapato kwa sekta ya madini yanatarajiwa kuongeza mapato
katika muda wa kati na mrefu.
22. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2010/11,
Serikali ilifanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa,
SURA 147 kwa kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta
mazito ya kuendeshea mitambo kutoka shilingi 97, hadi shilingi
80 kwa lita moja, ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa
nchini, katika kuzingatia dhamira ya Serikali ya kukuza viwanda,
33
kuongeza ajira na mapato ya ndani. Aidha, katika kipindi hicho,
Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria ya Magari SURA 124
pamoja na Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168 kwa
kupandisha ada ya usajili, uhamisho wa umiliki na ada ya mwaka
ya leseni za magari ili kuongeza mapato.
23. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia matakwa ya Itifaki ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwaka 2010/11 Mawaziri wa Fedha
wa Nchi wanachama waliridhia kufanya marekebisho mbalimbali
katika Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya
mwaka 2004 ili kuboresha sekta za viwanda, kilimo na
usafirishaji kama vichocheo muhimu katika kukuza uchumi wa
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
24. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2010 hadi
Machi 2011 mapato ya ndani, yakijumuisha mapato ya Serikali
za Mitaa, yalifikia shilingi bilioni 4,256.3, sawa na asilimia 69 ya
34
lengo la bajeti ya mwaka 2010/11 la shilingi bilioni 6,176.2. Kati
ya fedha hizo, shilingi bilioni 3,910.6 ni mapato ya kodi, shilingi
bilioni 227.4 ni mapato yasiyo ya kodi na mapato ya Serikali za
Mitaa yalikuwa shilingi bilioni 118.2.
25. Mheshimiwa Spika, mapato halisi ya ushuru wa forodha
yalikuwa shilingi bilioni 343.2, sawa na asilimia 70 ya lengo la
mwaka la kukusanya shilingi bilioni 493.1. Mapato kutokana na
ushuru wa bidhaa kutoka nje yalifikia shilingi bilioni 455.0, sawa
na asilimia 73 ya bajeti ya shilingi bilioni 622.8, wakati shilingi
bilioni 258.7, zilikusanywa kutokana na ushuru wa bidhaa
zilizozalishwa nchini, ikilinganishwa na bajeti ya shilingi bilioni
404.2, sawa na asilimia 64. Aidha, mapato kutokana na Kodi ya
Ongezeko la Thamani kutoka nje yalifikia shilingi bilioni 664.6,
ikilinganishwa na bajeti ya shilingi bilioni 999.3, sawa na asilimia
67, wakati shilingi bilioni 611.2 zilikusanywa kutokana na Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwa mauzo ya ndani, ikilinganishwa na
35
bajeti ya shilingi bilioni 992.3 sawa na asilimia 62. Makusanyo
halisi yanayotokana na Kodi ya Mapato yalikuwa shilingi bilioni
1,255.8, ikiwa ni asilimia 74 ya bajeti ya shilingi bilioni 1,702.3.
Aidha, mapato halisi yatokanayo na vyanzo vingine vya kodi
yalikuwa shilingi bilioni 449.7, ikiwa ni asilimia 72 ya bajeti ya
shilingi bilioni 620.9.
26. Mheshimiwa Spika, mapato yasiyo ya kodi kwa kipindi
cha Julai 2010 hadi Machi 2011, yalikuwa shilingi bilioni 227.4,
ikilinganishwa na bajeti ya shilingi bilioni 365.0, sawa na asilimia
62. Aidha, mapato ya Serikali za Mitaa yalikuwa shilingi bilioni
118.2, sawa na asilimia 68 ya bajeti ya shilingi bilioni 172.6.
MIKOPO YA NDANI:
27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Serikali
ilipanga kukopa shilingi bilioni 1,397.6, kutoka vyanzo vya ndani
36
ili kugharamia bajeti yake. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni
600.0 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na shilingi
bilioni 797.6 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani zitakazoiva. Hadi
Machi 2011, kiasi cha shilingi bilioni 1,107.5 kilikopwa kwa ajili
hiyo. Kiasi hiki kinajumuisha dhamana za Serikali zenye thamani
ya shilingi bilioni 607.6 zilizouzwa katika soko ili kulipia zilizoiva
na shilingi bilioni 499.9 zilitumika kugharamia miradi ya maendeleo.
MISAADA NA MIKOPO YA MASHARTI NAFUU KUTOKA
NJE:
28. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Mikopo, Dhamana na
Misaada ya mwaka 1974 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2004)
na Kanuni zake, imeendelea kuwa msingi na nguzo kuu ya
ukopaji mikopo, utoaji dhamana na kupokea misaada ikiwemo
misamaha/ unafuu wa madeni.
37
29. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2010 hadi
Machi 2011, misaada na mikopo ya kibajeti ilikuwa shilingi bilioni
845.7, sawa na asilimia 103 ya makadirio. Ongezeko hili
limetokana na nchi ya Canada kuongeza mchango wake wa
misaada ya kibajeti mara mbili ya makadirio ya awali. Misaada
na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikijumuisha mifuko
ya kisekta ilifikia shilingi bilioni 1,427.6, sawa na asilimia 58 ya
makadirio.
TATHMINI YA UWEZO WA NCHI KUKOPA NA KULIPA
MADENI (SOVEREIGN CREDIT RATING):
30. Mheshimiwa Spika, kufuatia kuanza kutengemaa kwa
uchumi wa dunia baada msukosuko wa kiuchumi duniani na nia
ya Serikali ya kuboresha upatikanaji wa taarifa zilizohakikiwa
kuhusu mwenendo mzuri wa Taifa kiuchumi, kisiasa, na utawala
bora. Serikali inaendelea kumtafuta Mshauri Mwelekezi wa
38
Kimataifa kwa ajili ya kusimamia zoezi la kutathmini uwezo wa
Nchi wa kukopa na kulipa madeni (Sovereign Credit Rating).
Mambo muhimu yanayozingatiwa katika tathmini hii ni pamoja
na; hali ya utulivu wa kisiasa; kasi ya kukua kwa uchumi;
udhibiti wa usimamizi wa bajeti ya Serikali; udhibiti wa masoko
ya fedha na hali ya mfumuko wa bei; na urari wa malipo ya nje
ya nchi. Hatua hii itasaidia kuwavutia wawekezaji na
wakopeshaji kutokana na kuwepo kwa taarifa ya hali ya uchumi,
siasa na utawala wa nchi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa
mikopo nafuu kutoka nje ya nchi kwa Serikali na kwa sekta
binafsi.
Deni la Taifa
31. Mheshimiwa Spika, mwaka 2000/01, Deni la Taifa,
lilikuwa Dola za Kimarekani bilioni 8.55 ikilinganishwa na Dola
bilioni 10.01 mwaka 2005/06 na kupungua mwaka 2006/07 hadi
39
kufikia Dola bilioni 7.53. Kupungua kwa deni hilo kulitokana na
misamaha mbalimbali ya madeni kutoka nchi wahisani na
mashirika ya fedha ya kimataifa chini ya utaratibu wa (HIPC na
MDRI). Aidha, Deni la Taifa liliongezeka hadi kufikia Dola bilioni
10.54 mwaka 2009/10, kutoka Dola bilioni 9.36 mwaka 2008/09.
Kati ya Deni la mwaka 2009/10, Dola bilioni 5.99 ni deni la nje
na Dola bilioni 4.55 ni deni la ndani, ikijumuisha Dola bilioni 1.63
za dhamana za Serikali kwa miradi ya Wizara, Idara na Taasisi za
Serikali.
Utegemezi wa Bajeti
32. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio niliyoyaeleza
kwenye mwenendo wa mapato hapo juu, Bajeti ya Serikali
imekuwa ikitegemea misaada ya wahisani, ambayo hivi sasa
(2010/11) ni asilimia 17 ya bajeti kutoka asilimia 28 mwaka
2007/08. Kwa kuzingatia umuhimu wa Taifa kujitegemea kifikra
40
na kirasilimali katika kuleta maendeleo, Serikali imeamua
kuchukua hatua madhubuti za kuongeza mapato ya ndani, ikiwa
ni pamoja na kupanua wigo, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji
na kutambua walipa kodi wapya; na kudhibiti matumizi ili ifikapo
mwaka 2015, kiwango cha utegemezi wa misaada ya wahisani
kwenye Bajeti ya serikali kisizidi asilimia 10.
MATUMIZI:
33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/11,
sera za matumizi ya Serikali zililenga katika kuboresha usimamizi
na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma ili kuongeza ufanisi
pamoja na kutoa kipaumbele kwa maeneo muhimu ya kiuchumi
yanayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini, hususan wa kipato. Katika kipindi cha Julai 2010 hadi
Machi 2011, jumla ya matumizi ilikuwa shilingi bilioni 7,169.3,
sawa na asilimia 67 ya makadirio ya mwaka. Kati ya fedha hizo,
41
shilingi bilioni 5,226.9 ni matumizi ya kawaida na shilingi bilioni
1,942.4 ni matumizi ya maendeleo.
34. Mheshimiwa Spika, hadi Machi 2011, malipo ya
mishahara ya watumishi wa Serikali yalikuwa shilingi bilioni
1,749.1, sawa na asilimia 79 ya Makadirio ya mwaka. Kati ya
fedha hizo, shilingi bilioni 569.96 zilitolewa kwa ajili ya Wizara na
Idara zinazojitegemea, shilingi bilioni 52.9 kwa ajili ya
Sekretarieti za Mikoa na shilingi bilioni 1,126.2 kwa ajili ya
Halmashauri. Aidha, jumla ya shilingi bilioni 443.9 zililipwa kwa
ajili ya mishahara ya taasisi na mashirika ya umma.
35. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai, 2010 hadi
Machi, 2011 malipo ya riba kwa madeni ya ndani yalifikia shilingi
bilioni 173.6, sawa na asilimia 74 ya makadirio ya mwaka. Aidha,
kiasi cha shilingi bilioni 44.6 kilitumika kulipia riba kwa madeni
ya nje, sawa na asilimia 34 ya makadiro ya mwaka. Kwa upande
42
wa madeni mengine (CFS Others), jumla ya shilingi bilioni 361.3
zilitumika ikiwa ni asilimia 66 ya makadirio ya mwaka na kiasi
cha shilingi bilioni 1,955.3 kilitumika kugharamia matumizi
mengineyo. Kwa ujumla, matumizi yalifanyika kulingana na
upatikanaji wa mapato.
36. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2010 hadi
Machi 2011, matumizi kwa ajili ya miradi ya maendeleo yalifikia
jumla ya shilingi bilioni 1,942.4, ambapo shilingi bilioni 514.8 ni
fedha za ndani na shilingi bilioni 1,427.6 ni fedha za nje,
ikilinganishwa na lengo la mwaka mzima la kutumia shilingi
bilioni 1,366.1 na bilioni 2,452.9, kwa mtiririko huo.
37. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa
vitambulisho vya Taifa, Serikali imekamilisha taratibu za kumpata
mzabuni na tayari mkataba umekwishasainiwa. Mradi huu
utagharimu jumla ya shilingi bilioni 355 mpaka utakapokamilika.
43
Kwa mwaka 2011/12, jumla ya shilingi bilioni 70 zitatumika
kama ilivyopangwa. Awamu ya kwanza ya uzalishaji wa
vitambulisho hivyo itakamilika mwishoni mwa mwaka 2011.
Mradi huu ukikamilika utawezesha wananchi kuwa na
utambulisho na hivyo kusaidia, pamoja na mambo mengine,
kuongeza wigo wa ulipaji kodi, kurahisisha upatikanaji wa
huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na huduma za kifedha, na
kuwatambua wahamiaji haramu.
MASUALA YANAYOHUSU SERIKALI ZA MITAA:
38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Serikali kuu
imeendelea kuzipa uwezo Serikali za mitaa wa kusimamia
rasilimali watu na fedha ili ziweze kutoa huduma kwa wananchi
kwa ufanisi. Aidha, Serikali imeendelea kuzipatia fedha,
watumishi na vitendea kazi na ushauri wa kitaalamu kulingana
na maeneo yaliyoainishwa kwenye bajeti. Hadi kufikia machi,
44
2011, Serikali za mitaa zilikuwa zimepokea jumla ya shilingi
bilioni 1,358.6, sawa na asilimia 90 ya lengo la shilingi bilioni
1,504.7 zilizotarajiwa kupelekwa kwa kipindi hicho.
39. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mapato ya ndani,
Serikali za mitaa, zimeendelea kukusanya mapato kutoka katika
vyanzo mbalimbali kwa mujibu wa sheria ya fedha za Serikali za
mitaa SURA 290. Katika mwaka wa fedha 2010/11, mapato
kutoka halmashauri yalikadiriwa kuwa shilingi bilioni 172.6. Hadi
kufikia mwezi Machi, 2011, mapato halisi yaliyokusanywa
kwenye halmashauri yalifikia jumla ya shilingi bilioni 118.2,
ambayo, ni sawa na asilimia 68 ya bajeti. Aidha, Serikali
imetekeleza majukumu mengi ikiwa ni pamoja na:
45
i) Kulipa kiasi cha shilingi bilioni 10.5 kwa ajili ya madeni ya
watumishi wa Serikali za Mitaa wasio walimu, kulingana na
uhakiki uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali;
ii) Ujenzi wa hospitali 3 za mikoa ya Manyara, Singida na
Mbeya, pamoja na ukarabati wa hospitali 10 za mikoa na
17 za wilaya;
iii) Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, nyumba 3 za
wakuu wa mikoa, ofisi 22 za Halmashauri na nyumba 210
katika Halmashauri mbalimbali;
iv) Ukarabati wa ofisi 17 za wakuu wa mikoa, ofisi 26 pamoja
na nyumba 23 za wakuu wa Wilaya; na
46
v) Kuboreshwa na kusambazwa kwa Mfumo wa IFMIS
(Integrated Financial Management Information System)
kwenye ngazi ya Halmashauri ili kuimarisha uwajibikaji,
ufuatiliaji na tathmini ya matumizi ya fedha za umma.
USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA:
40. Mheshimiwa Spika, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2009/10, inaonesha
kutetereka kwa udhibiti na usimamizi wa fedha za umma katika
Wizara, Idara na Sekretarieti za Mikoa, ikilinganishwa na taarifa
ya mwaka 2008/09. Taarifa inaonesha kupungua kwa Hati safi
za ukaguzi zilizotolewa kwa Wizara na Idara za Serikali, kutoka
asilimia 87 hadi asilimia 77, wakati hati zenye shaka
zimeongezeka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 20. Aidha, kwenye
Mamlaka za Serikali za Mitaa, hati safi za ukaguzi zimepungua
kutoka asilimia 58 mwaka 2008/09, hadi 48.5 mwaka 2009/10,
47
wakati hati zenye mashaka zimeongezeka kutoka asilimia 41
hadi asilimia 48.5.
41. Mheshimiwa Spika, baadhi ya sababu za kupungua kwa
hati safi za ukaguzi ni kutofuatwa kikamilifu kwa Viwango vya
Kimataifa vya utoaji wa taarifa za kihasibu katika Sekta ya
Umma (IPSAS), Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 na
kanuni zake za mwaka 2005, kukosekana kwa usimamizi na
ufuatiliaji wa karibu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,
kutozingatiwa kwa mfumo wa udhibiti wa ndani, ukosefu wa
mafunzo endelevu kwa watumiaji wa mfumo wa IFMIS kwenye
Serikali za Mitaa na kutotekelezwa kwa mapendekezo ya ukaguzi
kwa miaka iliyopita.
48
Usimamizi na Udhibiti wa Fedha za Umma - Serikali za
Mitaa
42. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi na
udhibiti wa fedha za umma, Sheria ya Fedha za Umma SURA
348 imepitiwa na kurekebishwa ili kuwapatia Mlipaji Mkuu wa
Serikali na Mhasibu Mkuu wa Serikali mamlaka ya kusimamia na
kufuatilia usimamizi wa fedha za umma katika ngazi ya Serikali
za Mitaa. Kupitia marekebisho haya, Serikali imeunda nafasi ya
Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi atakayeshughulikia usimamizi
wa fedha katika Serikali za Mitaa, na hivyo kuwezesha
utekelezaji wa dhima ambayo imekusudiwa na mabadiliko haya.
Usimamizi wa Mashirika ya Umma
43. Mheshimiwa Spika, katika miaka ya hivi karibuni,
zimejitokeza changamoto nyingi katika kusimamia wakala, taasisi
49
na mashirika ya umma. Baadhi ya mashirika na taasisi za umma
zinazotakiwa kujiendesha kibiashara zimeshindwa kujiendesha
kwa ufanisi na kuwa mzigo mkubwa kwa kutegemea ruzuku
kutoka Serikali Kuu, kinyume na lengo la kuanzisha mashirika na
taasisi hizo.
44. Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto hizo,
Serikali imefanya mabadiliko katika muundo wa Wizara ya
Fedha kwa kuifanya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwa wakala
anayejitegemea, kwa lengo la kuzisimamia kwa karibu wakala,
taasisi na mashirika ya umma na hivyo kuongeza ufanisi, tija,
mapato na kupunguza utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali
Kuu. Serikali inapitia sheria zilizoanzisha mashirika na taasisi
mbalimbali na sheria nyinginezo zinazohusiana na Ofisi ya
Msajili wa Hazina, ili kuondoa muingiliano wa kiutendaji.
50
MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI
(MKUKUTA II):
45. Mheshimiwa Spika, Serikali ilikamilisha maandalizi ya
MKUKUTA Awamu ya Pili (MKUKUTA II) na kuanza kutekelezwa
mnamo Julai 2010. Kama nilivyojulisha Bunge lako Tukufu katika
kikao cha bajeti mwaka 2010/11, MKUKUTA II ni nyenzo kuu ya
kuliwezesha Taifa kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi. Serikali inaendelea
kutenga fedha kwa ajili ya kugharimia MKUKUTA II hasa kwa
vipaumbele vinavyogusa wananchi walio wengi na kuboresha
huduma za jamii. Ugharamiaji wa Mkakati huu unategemea
bajeti ya Serikali, michango ya jamii na sekta binafsi.
46. Mheshimiwa Spika, MKUKUTA II umejikita katika maeneo
muhimu yafuatayo:
51
i) Miundombinu hususan, barabara za vijijini, reli, bandari,
viwanja vya ndege, nishati ya umeme na miundombinu
ya mawasiliano na habari pamoja na usafirishaji wa
nishati ya mafuta na gesi;
ii) Sekta ya Kilimo ikiwa ni pamoja na maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi;
iii) Sekta ya Viwanda, lengo likiwa kuendeleza viwanda
vitakavyotumia rasilimali za ndani; na
iv) Dhana ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi,
kwa maana ya kupanua na kuimarisha ushiriki na
mchango wa sekta binafsi katika maeneo ya
miundombinu, uzalishaji wa mazao ya chakula, biashara
pamoja na utoaji wa huduma za jamii kama vile afya,
usafirishaji, elimu na mafunzo na huduma za kifedha.
52
Tume ya Pamoja ya Fedha
47. Mheshimiwa Spika, Tume ya Pamoja ya Fedha ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliundwa kwa mujibu wa
Ibara ya 134 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Sheria ya Tume ya Pamoja ya Fedha SURA 140. Tume imetoa
taarifa kadhaa na mapendekezo ikiwemo taarifa iliyotolewa
mwaka 2006, kuhusu vigezo vya kugawana mapato na
kuchangia gharama za muungano. Taarifa hiyo imefanyiwa
mapitio mwaka 2010, ili kuiboresha na imewasilishwa kwa
Wizara ya Fedha ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Wizara
ya Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo ya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar mwezi April 2011. Kila upande
unaendelea kufanya uchambuzi wa mapendekezo ya Tume na
utawasilisha maoni yake katika kikao cha pamoja, chini ya
uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mapema mwaka 2011/12.
53
UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI:
48. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/2011, Serikali
iliendelea kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi, kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kupitia
mifuko na program mbalimbali; kuhamasisha uanzishwaji wa
vyama vya ushirika (SACCOS) na VICOBA kama njia bora ya
kupata mikopo yenye masharti nafuu, kuongeza kipato, ajira na
kupunguza umaskini. Matokeo ya uhamasishaji huo ni
kuongezeka kwa vyama hivyo mara tatu kutoka 1,875 mwaka
2005 hadi 5,344 mwaka 2010, na kuongezeka kwa idadi ya
wanachama wa vyama hivyo kutoka 1,360,850 hadi 2,100,000.
Akiba na amana za wanachama zimeongezeka zaidi ya mara
tano, kutoka shilingi bilioni 31.4 mwaka 2005, hadi shilingi bilioni
174.6 mwaka 2010. Aidha, Serikali imekamilisha Mwongozo wa
Ufuatiliaji na Tathmini ya Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya
54
Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. Vile vile, maandalizi ya
Mwongozo wa Kitaifa wa Kutoa Mafunzo ya Ujasiriamali
yanaendelea.
49. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012, Serikali
itaendelea kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wa Wananchi
Kiuchumi, kwa kuieneza ili wananchi wengi waielewe na kushiriki
kikamilifu katika utekelezaji wake; kutoa mafunzo kwa
wajasiriamali; kuhamasisha uwekaji akiba, uwekezaji na
kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika; na kufanya
tafiti zenye lengo la kuendeleza stadi za ujasiriamali na
kuanzisha na kuboresha shughuli za kiuchumi. Serikali itaendelea
pia kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za
maendeleo kupitia utaratibu unaosimamiwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii - TASAF.
55
MWELEKEO WA BAJETI YA MWAKA 2010/11 HADI JUNI,
2011:
50. Mheshimiwa Spika, kulingana na mwenendo wa
makusanyo ya mapato kwa kipindi cha miezi tisa ya mwaka
2010/11, inategemewa kwamba hadi kufikia Juni, 2011 Serikali
itaweza kukusanya jumla ya shilingi bilioni 5,553.7, sawa na
asilimia 93 ya lengo la shilingi bilioni 6,003.6.
51. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mikopo na misaada
ya kibajeti, hadi kufikia Juni 2011, kiasi cha shilingi bilioni 927.9
zinakadiriwa kupatikana, ikilinganishwa na shilingi bilioni 821.6
zilizokadiriwa hapo awali sawa na ongezeko la asilimia 13.
Mwelekeo unaonesha kwamba, hadi kufikia Juni 2011 sehemu
kubwa ya fedha zilizokadiriwa kupatikana kutokana na misaada
na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo zitapatikana.
56
52. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, Serikali
imeendelea kutoa fedha kulingana na upatikanaji wa mapato na
kwa kuzingatia vipaumbele vilivyopangwa. Mwelekeo ni kwamba
matumizi yatakuwa chini ya lengo la bajeti ya mwaka 2010/11
kutokana na upungufu wa mapato. Aidha, kabla ya mwisho wa
mwaka 2010/11, Serikali italipa madeni yaliyohakikiwa ya
vyombo vya dola ikiwa ni pamoja na posho ya nyumba kwa
Wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma na pango la nyumba kwa
Waheshimiwa Majaji.
MISINGI NA SHABAHA ZA BAJETI KWA MWAKA
2011/2012:
53. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2011/12 inazingatia
maeneo muhimu ya utekelezaji ili kufikia malengo ya Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2025, Awamu ya Pili ya Mkakati wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA II); Malengo ya
57
Maendeleo ya Milenia 2015; Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010-2015; Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania
(MPAMITA) na Mkakati wa Taifa wa Madeni.
54. Mheshimiwa Spika, maeneo muhimu yatakayozingatiwa
katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/12 ni kama
ifuatavyo:
i) Kukabiliana na changamoto za kupunguza makali ya
maisha kwa wananchi kama nilivyoeleza hapo awali;
ii) Kuendelea kuboresha mfumo wa makusanyo ya mapato
ya ndani, kuboresha mazingira ili kuvutia wawekezaji wa
ndani na nje na uendelezaji wa sekta binafsi ili kupanua
wigo na kuongeza vyanzo vipya vya mapato;
58
iii) Kuendelea na utekelezaji wa mradi wa Vitambulisho
vya Taifa; uanzishwaji wa anuani za makazi na
utekelezaji wa MKURABITA;
iv) Kuhakikisha kwamba maduhuli ya Serikali
yanakusanywa ipasavyo na kuwasilishwa katika Mfuko
Mkuu wa Serikali;
v) Kutenga rasilimali katika maeneo ya kuongeza kasi ya
ukuaji uchumi kama vile miundombinu ya umeme,
maji, barabara, bandari, kilimo, umwagiliaji, pamoja
na TEHAMA;
vi) Kuimarisha utawala bora na uwajibikaji;
59
vii) Kuendelea kutekeleza mipango na mikakati maalum ya
kuharakisha ukuaji wa uchumi, kama vile kuvutia
wawekezaji kwenye miradi ya uzalishaji kwa ajili ya
kuuza nje (EPZ) na wa uanzishaji wa maeneo maalum
ya uwekezaji (SEZs);
viii) Kukamilisha uandaaji wa awamu ya nne ya programu
ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma
(PFMRP IV);
ix) Kuimarisha uandaaji na utekelezaji wa sera za fedha
ziendane na zile za mapato na matumizi ili kupunguza
mfumuko wa bei na ongezeko la riba pamoja na
kuongeza mikopo kwa sekta binafsi na kuhakikisha
uhimilivu katika deni la Taifa;
60
x) Kuimarisha urari wa malipo kwa kusindika bidhaa
kabla ya kusafirishwa nje, hasa mazao ya kilimo,
madini na bidhaa nyingine;
xi) Kutafuta mikopo ya masharti nafuu na ya kibiashara
kutoka benki mbalimbali ili kuongeza uwezo wa
Serikali kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo;
xii) Kuharakisha utekelezaji wa Sheria ya Ubia kati ya
Sekta ya Umma na ya Binafsi ili kupanua fursa za
utekelezaji wa miradi ya maendeleo;
xiii) Kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya Sensa ya Watu
na Makazi ya mwaka 2012; na
61
xiv) Kulinda na kudumisha mafanikio yaliyopatikana katika
Sekta za huduma za jamii (Elimu, Maji na Afya).
SERA ZA MAPATO:
55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/12, Sera za
mapato zinalenga kukusanya mapato ya ndani, yasiyopungua
shilingi bilioni 6,775.9, sawa na asilimia 17.2 ya Pato la Taifa,
ikilinganishwa na matarajio ya kukusanya shilingi bilioni 5,553.7
au asilimia 16.0 ya Pato la Taifa kwa mwaka 2010/11. Kati ya
kiwango hicho, mapato ya kodi ni shilingi bilioni 6,228.8, mapato
yasiyo ya kodi ni shilingi bilioni 547.1 na mapato kutokana na
vyanzo vya Halmashauri ni shilingi bilioni 350.5.
56. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuimarisha
ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuchukua hatua mbalimbali
za kiutawala kwa kuhusisha maeneo ya mapato ya kodi na
62
yasiyo ya kodi, pamoja na kupanua wigo wa mapato katika
maeneo mengine. Maeneo ya kisera yatakayozingatiwa ili
kuongeza mapato ni pamoja na: -
i) Kuimarisha utaalamu na mbinu za kuhakiki kodi kutoka
kwenye kumbukumbu za biashara (audit capacity);
kuimarisha mfumo wa utawala wa kodi kwa kutumia
vitalu (Block Management System); kuingiza sekta isiyo
rasmi kwenye mfumo wa kodi; kutekeleza utawala wa
kodi kwa kutumia mfumo wa viashiria hatarishi
(Enterprise wide Risk Management); na kudhibiti mbinu
zote za ukwepaji Kodi;
ii) Kuhuisha Sheria mbalimbali zinazoruhusu misamaha ya kodi
kwa nia ya kudhibiti misamaha hiyo. Kwa sasa misamaha hiyo
ni asilimia 2.5 ya Pato la Taifa na lengo ni kufikia
angalau asilimia 1 ya Pato la Taifa katika muda wa kati;
63
iii) Kuendelea kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa
mapato kwa kuhakikisha kuwa malipo yanafanyika
kupitia benki; na kuanza kutumia mfumo wa kulipa kodi
kwa kutumia mfumo wa M-PESA kwa malipo ya Kodi
yasiyozidi shilingi 500,000 ili kuondoa kero ya walipa
kodi kukaa kwenye mistari;
iv) Kuimarisha TEHAMA katika utawala wa kodi – hasa
katika utozaji kodi kwenye sekta za Mawasiliano na
Fedha, ukaguzi wa kina (Forensic Audit), na utunzaji na
uchambuzi wa takwimu;
v) Kuendelea kuimarisha matumizi na udhibiti wa Mashine
za Elektroniki za kutoa stakabadhi za kodi (Electronic
Fiscal Devices-EFDs) na kutoa elimu kwa walipakodi na
wafanya biashara kuhusu matumizi ya mashine hizi;
64
vi) Kusimamia Mpango wa tatu wa Miaka Mitano wa
Maboresho ya utendaji wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi katika
kukusanya mapato;
vii) Kuboresha Mifumo ya Ukusanyaji na Usimamiaji kwa
Mapato yasiyo ya Kodi kwa kupitia upya mfumo wa
utoaji stakabadhi na leseni, pamoja na kuboresha
viwango vya kubakiza maduhuli (retention) kwa Wizara,
Idara na Taasisi za Serikali;
viii) Kupitia upya mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya
majengo (Property tax) katika majiji, manispaa, miji,
wilaya na miji midogo na kuboresha mfumo wa
ukusanyaji wake, kwa kutumia taarifa mpya za thamani
za majengo hayo na kusimamia ulipaji wa kodi hiyo,
65
ikiwa ni pamoja na kupitia upya vyanzo vya mapato na
mfumo wa ukusanyaji katika Serikali za Mitaa;
ix) kuendelea kuimarisha uchumi tulivu na kuweka
mazingira bora ya biashara ili kuwezesha sekta binafsi
kukua na hatimaye kuweza kuchangia katika mapato;
x) Kuimarisha miundombinu ya bandari, reli na barabara
ili kuchochea biashara na hatimaye kuongeza mapato;
na
xi) kuimarisha usimamizi na udhibiti wa bidhaa zipitazo
katika bandari zetu kwenda nchi za jirani, hasa bidhaa
za mafuta, ili kuzuia uvujaji wa mapato ya serikali.
66
MISAADA NA MIKOPO:
57. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2011/12,
Serikali inatarajia kupokea jumla ya misaada na mikopo yenye
masharti nafuu kiasi cha shilingi bilioni 3,923.6, ikilinganishwa na
kiasi cha shilingi bilioni 3,274.6 kwa mwaka 2010/11. Hili ni
ongezeko la shilingi bilioni 648.99, sawa na asilimia 20,
ukilinganisha na kiwango cha mwaka 2010/11. Kati ya fedha
hizo, shilingi bilioni 869.4 ni misaada na mikopo ya kibajeti na
shilingi bilioni 3,054.1 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi
ya maendeleo ikijumuisha mifuko ya kisekta.
58. Mheshimiwa Spika, napenda kuwatambua na
kuwashukuru washirika wetu wa maendeleo ambao
wameendelea kutoa misaada na mikopo kwa ajili ya maendeleo
ya nchi yetu licha ya nchi zao kuathirika na msukosuko wa
uchumi Duniani. Wahisani hao ni: Uingereza, Denmark, Uholanzi,
67
Ubelgiji, Canada, China, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland,
Italia, Japani, Korea ya Kusini, Norway, Sweden, Uswisi,
Marekani, India, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika,
BADEA, Umoja wa Ulaya, Global Fund, Shirika la Fedha la
Kimataifa (IMF), Kuwait Fund, Nordic Fund, Opec Fund, Saudi
Fund, na Mashirika ya Umoja wa Mataifa. Wote tunawashukuru
sana kwa michango yao.
MIKOPO YA KIBIASHARA:
59. Mheshimiwa Spika, kiwango cha mikopo yenye masharti
ya kibiashara kinazingatia tathmini ya uhimilivu wa deni la Taifa,
ambapo kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 1,500 zinakadiriwa
kukopwa kwa muda wa miaka mitatu, 2010/11 – 2012/13.
Hivyo, Dola za Kimarekani milioni 822, sawa na shilingi bilioni
1,271.6. zinatarajiwa kutumika mwaka 2011/12. Kati ya kiasi
68
hiki, Dola milioni 297 sawa na shilingi bilioni 459 ni albaki ya
mikopo iliyotarajiwa mwaka 2010/11 na Dola milioni 525, sawa
na shilingi bilioni 812 zinatarajiwa kupatikana mwaka 2011/12.
Fedha hizi zitatumika kwa miradi ya maendeleo ikijumuisha
miradi ya miundombinu.
MIKOPO YA NDANI:
60. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/12, Serikali
inakusudia kukopa kiasi cha shilingi bilioni 1,204.3 katika soko la
fedha la ndani. Kati ya kiasi hiki, shilingi bilioni 393.4 kwa ajili ya
kuziba nakisi ya mapato ya Serikali na kiasi cha shilingi bilioni
810.9 ni kwa ajili ya kulipia dhamana zinazoiva.
69
SERA ZA MATUMIZI
61. Mheshimiwa Spika, sera za matumizi ya Serikali
zinalenga katika kuboresha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya
fedha za umma, yakijumuisha udhibiti wa ulipaji wa mishahara,
matumizi katika miradi ya maendeleo, ruzuku ya pembejeo,
ununuzi wa umma na kuendelea kudhibiti ulimbikizaji wa
madeni. Msisitizo utawekwa kwenye kutekeleza maeneo
yaliyoainishwa kwenye misingi na shabaha za bajeti ya mwaka
2011/12, ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza
umasikini.
62. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maeneo ya
kipaumbele niliyoyaainisha katika aya ya 9, mchanganuo wa
bajeti kwa baadhi ya sekta kwa mwaka 2011/12 ni kama
ifuatavyo:
70
i) Miundombinu ya barabara, reli, bandari na Mkongo wa
Taifa zimetengewa shilingi bilioni 2,781.4
ikilinganishwa na shilingi bilioni 1,505.1 mwaka
2010/11 sawa na ongezeko la asilimia 85;
ii) Nishati na madini imetengewa shilingi bilioni 539.3
ikilinganishwa na shilingi bilioni 327.2 mwaka 2010/11,
sawa na ongezeko la asilimia 65;
iii) Maji imetengewa shilingi bilioni 621.6 ikilinganishwa
na shilingi bilioni 397.6 mwaka 2010/11, sawa na
ongezeko la asilimia 56;
iv) Kilimo na umwagiliaji kimetengewa shilingi bilioni
926.2 ikilinganishwa na shilingi bilioni 903.8 mwaka
2010/11, sawa na ongezeko la asilimia 2.5;
71
v) Elimu imetengewa shilingi bilioni 2,283.0
ikilinganishwa na shilingi bilioni 2,045.4 mwaka
2010/11, sawa na ongezeko la asilimia 12; na
vi) Afya imetengewa shilingi bilioni 1,209.1 ikilinganishwa
na shilingi bilioni 1,205.9 mwaka 2010/11, sawa na
ongezeko la asilimia 0.3.
Kudhibiti Matumizi
63. Mheshimiwa Spika, Serikali itahakikisha kwamba taratibu
za kifedha na ununuzi wa umma zinafuatwa kikamilifu pamoja
na kuondokana na matumizi yasiyokuwa ya lazima:-
a) Katika mwaka wa fedha wa 2011/12, Serikali itaendelea
kuchukua hatua mbalimbali za udhibiti wa matumizi, ikiwa
72
ni pamoja na kuimarisha ukaguzi wa mishahara, (Payroll
Audit) ambapo Maafisa Masuuli watafanya ukaguzi wa
malipo ya mishahara ya asasi/taasisi zao kila mwezi. Chini
ya utaratibu huu wakuu wa Idara watawajibika pia kufanya
ukaguzi wa mishahara ili kuhakikisha kuwa watumishi
wanaolipwa mishahara ni wale walio chini yao. Wakuu wa
Idara na Maafisa Wahasibu watawajibika kwa malipo ya
mishahara hewa. Aidha, Serikali itaendesha ukaguzi wa
mara kwa mara kwa malipo ya mishahara kupitia Idara ya
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali na pia kupitia Sehemu
ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Serikali na Utendaji Kazi
katika Idara ya Bajeti ya Serikali. Katika mwaka 2011/12,
Serikali imepanga kufanya sensa ya watumishi wote wa
Serikali na Taasisi kwa kuandaa siku maalum ya malipo ya
mshahara dirishani “National Pay Day”. Aidha, Serikali
itasimamia utekelezaji wa Waraka Na. 2 wa Hazina wa
mwaka 2010 kuhusu uwajibikaji na udhibiti katika
73
usimamizi wa malipo ya mishahara pamoja na ukamilishaji
wa maboresho ya mfumo wa kuandaa mishahara (Lawson,
version 9), ambao utaimarisha udhibiti wa malipo ya
mshahara.
b) Eneo lingine ambalo litazingatiwa ni ukaguzi wa miradi ya
maendeleo. Kazi hii itafanywa na Kitengo cha Ukaguzi wa
Kiufundi (Technical Audit Unit) ambacho kitakuwa chini
ya Idara mpya ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.
Ukaguzi huu utajikita katika kuhakikisha kuwa matumizi
ya fedha katika miradi husika, yanaendana na thamani
halisi ya fedha iliyotumika (Value for Money).
c) Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali aliyoitoa mwezi Machi 2011 imeonesha kuwa
kuna udhaifu mkubwa wa usimamizi wa fedha za umma
74
katika Serikali za Mitaa. Katika jitihada za kukabiliana na
hali hii, Serikali inaendelea kupunguza idadi ya Akaunti
za Benki katika Halmashauri hadi zifikie sita. Hivyo,
kuanzia tarehe 1 Julai, 2011 Serikali za Mitaa zitakuwa na
akaunti zifuatazo: Akaunti ya Mapato, Akaunti ya Amana,
Akaunti ya Mishahara, Akaunti ya Matumizi ya Kawaida,
Akaunti ya Matumizi ya Maendeleo na Akaunti ya Mfuko
wa Barabara. Hatua hii itasaidia kudhibiti matumizi ya
fedha, kuongeza uwazi na uwajibikaji na kuboresha
utoaji wa taarifa za mapato na matumizi. Aidha, Serikali
imeendelea kuimarisha mfumo wa uwajibikaji na
ufuatiliaji katika Serikali za Mitaa ili kupata thamani
stahiki ya fedha za umma. Vilevile, Mkaguzi Mkuu wa
Ndani wa Serikali, pamoja na mambo mengine, atakuwa
na majukumu ya kusimamia masuala ya ukaguzi wa
ndani katika Serikali za Mitaa.
75
d) Kila mwaka Serikali inatumia sehemu kubwa ya bajeti
yake katika ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali.
Hivyo, katika mwaka wa fedha 2011/12, Serikali
imedhamiria kuweka mfumo wa ununuzi wa umma
unaowezesha Serikali na Taasisi zake kupata bidhaa na
huduma zenye ubora unaotakiwa kwa bei nzuri. Aidha,
Serikali itaendelea na juhudi zake za kudhibiti matumizi
yake kwa kusitisha ununuzi wa magari ya aina zote
isipokuwa kwa sababu maalum na kwa kibali cha ofisi ya
Waziri Mkuu. Vile vile, Serikali itasitisha ununuzi wa
samani za ofisi hususan zile zinazoagizwa nje ya nchi;
kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na
tija; kupunguza matumizi ya mafuta kwa magari ya
Serikali; kupunguza safari za ndani na nje ya nchi ikiwa ni
pamoja na ukubwa wa misafara; na pia kuendelea
kupunguza uendeshaji wa semina na warsha isipokuwa
pale inapobidi na kwa kibali cha Ofisi ya Waziri Mkuu;
76
pamoja na kupunguza gharama za maonesho na sherehe
mbalimbali.
e) Tangu kutungwa kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma SURA
410 yamejitokeza mapungufu mbalimbali katika
utekelezaji wa Sheria hii. Mapungufu hayo ni pamoja na
yale yaliyobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Serikali ya mwaka 2009/10, ambapo baadhi ya
Idara na taasisi za Umma zimeonesha udhaifu katika
utekelezaji wa Sheria hii. Aidha, ili kushughulikia
mapungufu haya, Serikali iliwasilisha Muswada wa Sheria
wenye mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya
Ununuzi wa Umma 2010 katika mkutano wa Bunge
uliofanyika mwezi Aprili mwaka huu. Muswada huu
ulijadiliwa na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi
pamoja na wadau mbalimbali, ambapo ilitolewa michango
77
ya kina yenye lengo la kuboresha Muswada. Serikali kwa
kuthamini michango hii, iliona ni vyema kuchapisha upya
Muswada huu na baada ya kukamilika kwa zoezi hili,
Serikali inatarajia kuuwasilisha Bungeni kwa ajili ya
kujadiliwa.
f) Kuendelea kuimarisha mtandao wa kompyuta wa mfumo
wa usimamizi wa fedha (IFMIS) katika ngazi zote za
Serikali kwa lengo la kudhibiti matumizi na kuzuia
malimbikizo ya madeni; kutoa mafunzo kwa wahasibu juu
ya uandaaji wa hesabu katika viwango vya kimataifa vya
uhasibu katika sekta ya umma (IPSAS) ili viweze
kuzingatiwa kikamilifu; kutumia utaratibu wa kufanya
malipo kwa kutumia TISS na kuanza kutumia utaratibu
huu wa malipo katika Ofisi za Hazina ndogo na Sekretarieti
za Mikoa.
78
g) Serikali itaendelea kudhibiti utoaji wa dhamana za Serikali
kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali. Aidha Wizara,
Idara na Taasisi za Serikali zinatakiwa kuomba fedha za
miradi mbalimbali kwa utaratibu wa kawaida wa kibajeti
na sio kwa utaratibu wa kuomba dhamana. Hatua hii
itasaidia kupunguza maombi ya dhamana ili kuepuka
ongezeko la deni la Taifa lisilohimilika.
Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
64. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/11,
Bunge lilipitisha Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi ya mwaka 2010 (Public Private Partnership Act Na.19 of
2010). Kupitia Sheria hii, Sekta Binafsi kwa kushirikiana na sekta
ya umma itaweza kujenga na kuendesha miradi muhimu na
kutoa huduma za kijamii na kiuchumi kama kilimo,
miundombinu, viwanda, madini, elimu, afya, mazingira,
79
TEHAMA, biashara, michezo na burudani; hivyo kutoa nafasi kwa
Serikali kuelekeza nguvu katika vipaumbele vingine. Aidha,
Sheria hii inakusudia kuwawezesha wananchi kupata huduma za
uhakika, endelevu, na kwa gharama nafuu, hivyo kuinua uchumi
wa nchi yetu kwa kasi kubwa.
65. Mheshimiwa Spika, miradi ya ubia itakuwa na faida
nyingi kwa taifa letu kama ifuatavyo:
i) Kuongeza ushindani katika soko la ajira na hivyo
kuchochea ufanisi;
ii) Kupanuka kwa biashara na kuongeza wigo wa kodi ya
mapato;
iii) Kutumia raslimali-fedha za sekta Binafsi ambazo kwa
kawaida ni nyingi na zinahitajika sana katika kuongeza
mzunguko wa fedha katika uchumi wa nchi;
80
iv) Kuipunguzia au kuiondolea mzigo Serikali wa kubeba
mashirika yasiyo na ufanisi na kuelekeza nguvu katika
vipaumbele vingine; na
v) Wananchi kupata uhakika wa huduma na kwa
gharama nafuu.
66. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Ubia kati ya sekta ya
Umma na sekta Binafsi, imeanzisha vitengo viwili. Kitengo kimoja
kiko Kituo cha Uwekezaji Tanzania ambacho kitahusika na
kutangaza na kutoa vivutio kwa wawekezaji. Kitengo cha pili kiko
Wizara ya Fedha ambacho kitahusika na kuifanyia tathmini
miradi ya ubia na kuhakikisha kuwa miradi inayoanzishwa hapa
nchini inajiendesha kibiashara, na kwa misingi ya thamani ya
fedha, na haisababishi mzigo kwa Serikali. Serikali inakusudia
kuvipatia vitengo hivi watalaam zaidi na wenye ujuzi wa fani ya
Ubia kimataifa.
81
Majadiliano kati ya Wizara na Kamati za Kisekta za
Bunge
67. Mheshimiwa Spika, katika mchakato wa kupitisha bajeti
katika baadhi ya kamati za Kisekta za Bunge, kulikuwa na maoni
kwamba bajeti za baadhi ya Sekta hizo zilizopangwa kwa mwaka
2011/12, ni ndogo na kutoa ushauri kwamba ziongezwe. Serikali
imetafakari hayo yote na imeazimia kufanya marekebisho kwa
baadhi ya mafungu ya bajeti kwa kuzingatia upatikanaji wa
mapato mapya. Marekebisho hayo yatawasilishwa bungeni kwa
ajili ya kuidhinishwa.
Maslahi ya Watumishi
68. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha maslahi
ya watumishi kulingana na uwezo wa mapato yake kwa lengo la
kuwawezesha kumudu gharama za maisha. Maeneo ambayo
yatatiliwa mkazo ni pamoja na malipo ya mshahara na likizo kwa
82
wakati, kuhakikisha watumishi wanalipwa mafao yao mara baada
ya kustaafu, pamoja na pensheni zao za kila mwezi. Sambamba
na hayo, Serikali itatoa mafunzo kwa maafisa wa Hazina ndogo
na wa mahakama zote zinazoshughulikia mirathi, na kuweka
mikakati ya pamoja kuwaondolea kero wasimamizi na warithi wa
mali ya marehemu.
Usimamizi wa Mashirika ya Umma
69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2011/12,
Ofisi ya Msajili wa Hazina, pamoja na mambo mengine, imelenga
kufanya yafuatayo katika usimamizi wa wakala, taasisi na
mashirika ya umma:
i) Kuwezesha wakala, taasisi na mashirika ya umma
kuingia mikataba ya utendaji na Wizara mama;
83
ii) Kutekeleza ukaguzi wa kimenejimenti kwa wakala,
taasisi na mashirika ya umma;
iii) Kuuandaa mfumo wa uperembaji na uhakiki wa
menejimenti na Bodi za wakala, taasisi na mashirika ya
umma;
iv) Kuongeza makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kwa
kuzingatia Sheria ya Fedha Na. 13 ya mwaka 2008
pamoja na Waraka wa Hazina Na. 8 wa 2008/09;
v) Kuunda Mfuko wa Uwekezaji kwa ajili ya mitaji ya
wakala, taasisi na mashirika ya umma;
vi) Kutathmini mfumo wa uwiano wa mishahara ya
wakala, taasisi na mashirika ya umma;
84
vii) Kuratibu uperembaji na uhakiki wa mashirika
yaliyobinafsishwa; na
viii) Kuendelelea kushauri Serikali juu ya uwekezaji katika
wakala, taasisi na mashirika ya umma.
MASUALA YANAYOHUSU SERIKALI ZA MITAA:
70. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha
utendaji na uwajibikaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia
Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP II) ili
kuwawezesha Wakurugenzi kusimamia majukumu yao kikamilifu.
Serikali pia itawajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani ili
wasimamie utendaji wa Halmashauri zao na kuhakikisha
nidhamu ya kazi inaimarishwa kulingana na sheria, taratibu na
kanuni za utumishi wa umma. Aidha, kamati za kupambana na
rushwa pamoja na kamati za maadili za Halmashauri
85
zitaimarishwa ili kusimamia nidhamu ya watumishi wa kada zote
na kuhakikisha utendaji wao unazingatia maslahi ya taifa. Vile
vile, Serikali itaimarisha mfumo wa tathimini ya utendaji kazi -
OPRAS kwa watendaji wa Halmashauri na kufanya mapitio ya
vigezo vya kupima utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri
(Peformance Assessment Criteria) ili kuongeza tija na ufanisi wa
watendaji wa Serikali za Mitaa.
71. Mheshimiwa Spika, Serikali za Mitaa zitaendelea
kukusanya mapato kutoka katika vyanzo vyake, ambapo jumla
ya shilingi bilioni 350.5 zinakadiriwa kupatikana kutoka vyanzo
hivyo. Kiwango hicho cha mapato ni sawa na asilimia 5.2 ya
mapato ya ndani yanayokusanywa na Serikali Kuu. Kiwango
hicho kinaonesha juhudi zitakazochukuliwa na Serikali kuboresha
ukusanyaji ikilinganishwa na asilimia 2.9 ya mapato ya ndani
yanayotarajiwa mwaka 2010/11. Serikali itaendeleza juhudi za
ukusanyaji mapato katika ngazi ya Halmashauri, ili kuhakikisha
86
kwamba mapato hayo yanawiana na fursa zilizopo. Baadhi ya
hatua zitakazochukuliwa, ni pamoja na: kuendelea kuboresha
mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato kutoka vyanzo
vya Halmashauri; kupitia upya vyanzo vya Halmashauri
vilivyofutwa; kupitia mfumo wa kodi ya majengo katika majiji,
manispaa, miji, wilaya na miji midogo; na kuainisha mianya ya
upotevu wa mapato na vyanzo mbadala vya kuongeza mapato
ya Serikali za Mitaa.
72. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, Serikali
itaendelea kuboresha uratibu na usimamizi wa matumizi ya
Halmashauri. Baadhi ya hatua zitakazotekelezwa ni pamoja na
kuziwezesha na kuziimarisha Idara za Mipango, uhasibu na
ukaguzi wa ndani ili kuongeza uwajibikaji, usimamizi na udhibiti
wa fedha katika Halmashauri; kuboresha na kupanua
miundombinu ya barabara, maji na umeme; kuendelea
kutekeleza sera ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi kwa
87
kujenga uwezo wa Halmashauri katika kusimamia utekelezaji wa
majukumu yao; na kuendelea kutekeleza program mbalimbali za
maboresho.
MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA, TOZO NA
HATUA NYINGINE ZA MAPATO:
73. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuchukua hatua
mbalimbali za kisera na kiutawala ili kuongeza mapato ya kodi
na yasiyo ya kodi, na kupanua wigo wa mapato katika maeneo
mengine. Aidha, Serikali itaendelea kufanya mapitio ya sheria
mbalimbali zinazotoa misamaha ya kodi kwa lengo la kudhibiti na
kupunguza misamaha hiyo; kusimamia Mpango wa tatu wa
Miaka Mitano wa Maboresho ya utendaji wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA); Kuendelea kuingiza Sekta isiyo rasmi kwenye
mfumo wa kodi; kupitia upya mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya
majengo katika majiji, manispaa, miji, wilaya na miji midogo; na
88
kufanya mapitio ya vyanzo vya mapato na mfumo wa ukusanyaji
katika Serikali za Mitaa ili kuongeza mapato.
74. Mheshimiwa Spika, marekebisho ya mfumo wa kodi
yanahusu sheria zifuatazo:-
a) Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148;
b) Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332;
c) Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
d) Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82;
e) Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189;
f) Sheria ya ushuru wa Mafuta ya Petroli, SURA 220;
g) Sheria ya Leseni za Biashara, SURA 208;
h) Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, SURA 290;
i) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168.
89
j) Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya sheria
za kodi;
k) Marekebisho ya Ada na Tozo Mbalimbali za Wizara,
Mikoa na Idara zinazojitegemea;
l) Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ya
mwaka 2004;
A. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148
75. Mheshimiwa Spika, ili kuhamasisha uwekezaji na
kuboresha uzalishaji katika Sekta za Kilimo, Mifugo, Viwanda,
Biashara na Utalii na kuziwezesha kuchangia zaidi kwenye pato
la Taifa, napendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya
Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 kama ifuatavyo: -
90
i) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye Vipuri
vya Zana za kilimo zifuatazo:- fyekeo (threshers),
mashine za kukausha na kukoboa mpunga (rice dryers
and mills), mashine za kupandia mbegu (planters), na
matrekta ya kukokota kwa mkono (power tillers).
ii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye chakula
cha kuku (NASCOR Pellet Feed). Hatua hii ina lengo la
kuhamasisha uwekezaji katika ufugaji wa kuku hapa
nchini;
iii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye nyuzi
(Nylon Fishing Twine) zinazotumika kutengeneza nyavu
za kuvulia samaki. Hatua hii inalenga katika kupunguza
gharama za uzalishaji na kuendeleza sekta ya uvuvi hapa
nchini;
iv) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vipuri
vya mashine za kunyunyiza na kutifua udongo (sprayers
91
and harrows) na mashine za kupanda nafaka (grain
conveyors); na
v) Kuanzisha utaratibu wa marejesho ya Kodi kwenye
mauzo ya rejareja kwa bidhaa za ndani zinazouzwa kwa
abiria ambao sio raia wa Tanzania wanaosafiri nje ya
nchi. Utaratibu huu utaanza kutekelezwa kwa kuanzia na
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro kwa mauzo ya thamani ya shilingi 400,000 na
zaidi. Utekelezaji wa utaratibu huu mpya utaanza rasmi
tarehe 1 Januari 2012.
76. Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanya
marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani,
SURA 148 kwa nia ya kuongeza mapato na kuhamasisha
Mashirika na Taasisi mbalimbali ziweze kuchangia katika juhudi
za serikali za kuboresha huduma katika sekta ya elimu.
92
vi) Kuondoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
kwenye kuuza na kupangisha majengo ya kuishi ya
nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC);
vii) Kuondoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
uliokuwa unatolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
(Non Governmental Organizations). Hatua hii haitazihusu
Taasisi za Kidini (Religious Organizations); na
viii) Kutoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa
Mashirika yasiyo ya kiserikali (Non Governmental
Organizations) kwa vifaa vya matumizi binafsi ya
kawaida (household consumables) kama vile vyakula,
mavazi, na vifaa kama sabuni ambavyo vinatolewa
93
msaada kwenye vituo mahsusi vya kulelea watoto yatima
na shule.
Hatua hizi katika Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa
pamoja zitaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha
shilingi milioni 71,518.9.
B. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332
77. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
ya sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: -
i) Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa
wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye
Taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya
Serikali..
94
ii) Kufuta Kodi ya Zuio kwa usafirishaji wa samaki nje ya nchi
kwa kutumia ndege za nje. Hatua hii inalenga katika
kuhamasisha mauzo ya samaki nje ya nchi.
Hatua hizi za Kodi ya Mapato zitapunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 20,287.5
C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
78. Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
i) Kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta mazito ya
kuendeshea mitambo kutoka shilingi 80 hadi shilingi 40
kwa lita ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa
hapa nchini;
95
ii) Kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 50 badala ya asilimia
120 kwenye mifuko ya plastiki za microns 30 na zaidi
yaani Polymers of ethylene na nyinginezo za (HS. Code
3923.2900).
iii) Kurekebisha kwa asilimia 10 viwango vya Ushuru wa
bidhaa mbalimbali isipokuwa zile za mafuta ya Petroli
kama ifuatavyo: -
a) Vinywaji baridi kutoka shilingi 63 kwa lita hadi shilingi 69
kwa lita;
b) Bia inayotengenezwa na nafaka ya hapa nchini na ambayo
haijaoteshwa, kutoka shilingi 226 kwa lita hadi shilingi 249
kwa lita;
c) Bia nyingine zote, kutoka shilingi 382 kwa lita hadi shilingi
420 kwa lita;
96
d) Mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya
nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, kutoka shilingi
1,223 kwa lita hadi shilingi 1,345 kwa lita;
e) Mvinyo uliotengenezwa kwa Zabibu inayozalishwa hapa
nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75 utatozwa
shilingi 420 kwa lita; na
f) Vinywaji vikali, kutoka shilingi 1,812 kwa lita hadi shilingi
1,993 kwa lita.
(iv) Kurekebisha viwango vya Ushuru wa bidhaa kwenye
sigara kama ifuatavyo: -
a) Sigara zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kutokana na
tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha
angalau asilimia 75, kutoka shilingi 6,209 hadi shilingi
6,830 kwa sigara elfu moja;
97
b) Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na
tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha
angalau asilimia 75, kutoka shilingi 14,649 hadi shilingi
16,114;
c) Sigara nyingine zenye sifa tofauti na (a) na (b) kutoka
shilingi 26,604 hadi shilingi 29,264 kwa sigara elfu moja;
d) Tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara (cut filler)
kutoka shilingi 13,436 hadi shilingi 14,780 kwa kilo; na
e) Ushuru wa (Cigar) unabaki asilimia 30.
Hatua hizi katika Ushuru wa Bidhaa kwa pamoja
zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 99,521.5
98
D. Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82
79. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
kwenye sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82
kama ifuatavyo:
i) Kufanya marekebisho katika mgawanyo wa mapato
yatokanayo na tozo ya kuendeleza ufundi stadi (Skills
Development Levy) ya asilimia 6 ili asilimia 4 zipelekwe
kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
na asilimia 2 zipelekwe Mamlaka ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi (Vocational Education and Training
Authority - “VETA”). Lengo la hatua hii ni kuongeza
fedha za mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Hatua hii katika Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
haitarajiwi kupunguza wala kuongeza mapato ya
Serikali.
99
E. Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189
80. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
ya Ushuru wa Stempu, SURA 189 kama ifuatavyo: -
i) Kusamehe ushuru wa stempu wakati umiliki wa mali
(Asset) unapohamishiwa katika chombo maalum
(Kampuni) cha kutekeleza na kusimamia uzalishaji wa
kipato (Special Purpose Vehicle “SPV”) kwa madhumuni
ya kutoa dhamana zinazotegemea hiyo mali ambayo
umiliki wake umehamishwa. Hatua hii inalenga katika
kuhamasisha miradi ya uwekezaji inayohitaji fedha
nyingi, mfano; miradi ya barabara, madaraja, nishati na
maji. Aidha, ni njia mbadala ya mabenki ya upatikanaji
wa fedha za kugharamia miradi.
Hatua hii ya ushuru wa stempu haitapunguza mapato
ya Serikali bali inalenga katika kuhamasisha utunzaji wa
100
akiba na kuchochea uwekezaji (Savings Mobilization and
Investment Promotion).
F. Sheria ya Ushuru wa Mafuta ya Petroli, SURA 220
81. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Ushuru wa mafuta ya petroli, SURA 220 kama
ifuatavyo:
i) Kusamehe Ushuru wa Mafuta ya Petroli unaotozwa kwenye
mafuta yanayotumika kwenye kuendesha meli, na vifaa
vingine vinavyotumika katika utafiti wa mafuta na gesi na
msamaha huu utatolewa kupitia Tangazo la Serikali. Aidha,
maombi ya msamaha yatahakikiwa na kupitishwa na Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kabla ya
kuwasilishwa Wizara ya Fedha. Hatua hii inalenga katika
kutoa unafuu wa gharama kwa Kampuni zinazofanya utafiti
wa mafuta na gesi.
101
ii) Ili kutatua tatizo la ucheleweshaji wa marejesho ya kodi (tax
refunds) kwenye mafuta yanayonunuliwa na Kampuni za
madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaanzisha
utaratibu wa kuweka kiasi cha fedha kwenye Akaunti
maalum (escrow account) ambacho kinawiana na kiwango
cha mahitaji ya mafuta kwa mwezi. Aidha Kampuni
itaruhusiwa kununua mafuta kwenye matanki ya Kampuni za
waagizaji wa mafuta bila ya kulipia kodi kwa kiwango cha
fedha ilichoweka kwenye akaunti. Endapo mahitaji ya mafuta
kwa mwezi yatakuwa makubwa zaidi ya kiwango ilichoweka
kwenye akaunti, Kampuni hiyo itawajibika kuongeza fedha za
ziada zenye kukidhi mahitaji yake. Hatua hii inatarajiwa
kutatua tatizo la ucheleweshaji wa marejesho ya kodi
iliyolipwa kwenye mafuta.
102
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaandaa utaratibu wa
utekelezaji utakaohusisha kampuni za madini na kampuni za
mafuta.
Hatua hizi kwa pamoja zitapunguza mapato ya Serikali kwa
shilingi milioni 2,007.6
G. Sheria ya Leseni ya Biashara, SURA 208
82. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Leseni ya Biashara, SURA 208 ili kutoza ada ya
leseni ya biashara kwa viwango na maeneo yafuatayo: -
a) Mamlaka za Miji (Majiji, Manispaa na Miji) zitoze shilingi
50,000 kwa mwaka kwa kila aina ya biashara inayostahili
103
kupewa leseni ya biashara (isipokuwa ya vileo)
inayoendeshwa katika maeneo ya mamlaka hizo.
b) Halmashauri za Wilaya zitoze na kukusanya Ada ya leseni
ya biashara ya shilingi 30,000 kwa mwaka kwa biashara
zinazoendeshwa katika maeneo ya miji midogo na vituo
vya biashara.
c) Halmashauri za vijiji zitoze na kukusanya shilingi 10,000
kwa mwaka kwa kila biashara inayoendeshwa katika
maeneo yake.
Lengo la hatua hii ni kuimarisha usimamizi wa Kanuni za
biashara hapa nchini na kuwianisha ukuaji wa biashara na
mapato yanayokusanywa. Pia itaongeza mapato kwa
Serikali za Mitaa na kuongeza uwezo katika kuhimili
mahitaji yao. Aidha, utekelezaji wa hatua hii unazingatia
Sera ya Serikali ya ugatuaji madaraka kwa wananchi
(Decentralization by Devolution “D by D”).
104
H. Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, SURA 290
83. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa SURA 290 ili
kuziwezesha Serikali za Mitaa kutoza ada ya leseni ya biashara
kwa viwango na maeneo yaliyoainishwa kwenye sheria ya leseni
ya biashara.
I. Sheria ya Usalama Barabarani, SURA168
84. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya
Sheria ya Usalama Barabarani, Sura, 168 ili kuongeza ukomo wa
kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa
uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka
shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.
105
J. Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria
za Kodi
85. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
mengine madogo madogo yasiyo ya kisera katika Sheria
mbalimbali za kodi ili ziwe sanjari na azma ya kurahisisha
utekelezaji wake.
K. Marekebisho ya Ada na Tozo Mbalimbali za Wizara,
Mikoa na Idara zinazojitegemea.
86. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
ya viwango vya ada na tozo mbali mbali zinazotozwa na Wizara,
Mikoa na Idara zinazojitegemea ili kuvihuisha kulingana na hali
halisi ya ukuaji wa uchumi.
106
L. Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ya
mwaka 2004
87. Mheshimiwa Spika, kikao cha maandalizi ya Bajeti cha
Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Pre-Budget
Consultations of EAC Ministers for Finance) kilichofanyika tarehe
7 Mei 2011 jijini Kampala, Uganda; kilipendekeza marekebisho
ya viwango vya Ushuru wa pamoja wa Forodha (EAC Common
External Tariff “CET”) na Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004). Marekebisho
hayo yanalenga katika kukuza Sekta za Viwanda, Usafirishaji,
Mifugo, Biashara na Utalii. Aidha yanalenga pia katika kuboresha
afya ya jamii na kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali
zao.
107
88. Mheshimiwa Spika, maeneo yanayopendekezwa
kufanyiwa marekebisho kwenye viwango vya Ushuru wa Pamoja
wa Forodha (EAC Common External Tariff) ni yafuatayo:-
i) Tanzania iruhusiwe kutoza ushuru wa forodha wa
asilimia 10 badala ya asilimia 35 kwenye ngano
inayotambuliwa katika HS Code 1001.90.20 na HS
Code 1001.90.90 kwa muda wa mwaka mmoja. Lengo
la hatua hii ni kupunguza gharama za uingizaji nchini
wa bidhaa hiyo na kuwezesha walaji kupata vyakula
kwa bei nafuu.
ii) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwenye malighafi ya kutengeneza sabuni
(Palm Stearin, RBD) inayotambuliwa katika HS Code
1511.90.40 kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hatua hii
inalenga kutoa unafuu wa kodi kwenye viwanda
108
vidogo na vya kati vya kutengeneza sabuni hapa
nchini.
iii) Kutenganisha malighafi zinazotambulika katika HS
Code 2710.19.59 ili kutoa msamaha wa ushuru wa
forodha (duty remission) kwenye malighafi za
kutengeneza manukato na sabuni (white oil). Hatua
hii inalenga katika kupunguza gharama za uzalishaji
viwandani.
iv) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwenye malighafi za kutengeneza maganda
ya viberiti (duplex boards) yanayotambuliwa katika HS
Code 4810.92.00. Hatua hii inalenga katika kupunguza
gharama za uzalishaji na kulinda Viwanda vya Viberiti
kutokana na ushindani wa viberiti vinavyoagizwa nje.
109
v) Kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya
asilimia 0 kwenye waya za chuma ambazo
zimenakisiwa na zink (Galvanized Plated/Coated Wire),
zinazotambuliwa katika HS Code 7217.20.00 kwa kuwa
waya ambazo hazikunakisiwa (Non Plated/Coated
Wire) hutozwa ushuru wa forodha wa asilimia 10.
Lengo la hatua hii ni kuwianisha ushuru wa malighafi
inayotumika kuzalisha bidhaa hii ili iendane na
kanuni/taratibu za kutoza ushuru zinazozingatia
viwango vya usindikaji.
vi) Kupunguza ushuru wa forodha kwenye mifuko ya
plastiki ya kuhifadhia malighafi za matunda (aseptic
bags) kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10
inayotambuliwa katika HS Code 3923.29.00 kwa
kipindi cha mwaka mmoja ili kupunguza gharama za
110
uzalishaji na kuhamasisha usindikaji wa mazao ya
matunda hapa nchini.
vi) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye shaba
ghafi (copper Cathodes) inayotambuliwa katika HS Code
7403.11.00. Hivi sasa bidhaa hii inatozwa ushuru wa
asilimia 10 ambapo shaba iliyotengenezwa kwa ukamilifu
(copper alloys/refined copper) hutozwa ushuru wa
asilimia 0, ambapo ni kinyume na matakwa ya sheria ya
ushuru wa forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya
mwaka 2004. Lengo la hatua hii ni kuwianisha ushuru wa
malighafi inayotumika kuzalisha bidhaa hii ili iendane na
kanuni/taratibu za kutoza ushuru zinazozingatia viwango
vya usindikaji.
111
viii) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwa waunganishaji wa majokofu
(refrigerators and freezers) ili walipe ushuru wa
forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 25 kwenye
vifaa vya kuunganisha majokofu hayo (component
parts and inputs for assemblers of refrigerators and
freezers). Hatua hii inalenga katika kuhamasisha
uzalishaji wa bidhaa hizo na kuongeza ajira hasa kwa
vijana.
ix) Kutenganisha malighafi zinazotambulika katika HS
Code 2309.90.00 ili kutoa msamaha wa ushuru wa
forodha kwenye malighafi za kutengeneza vyakula vya
mifugo (premixes). Lengo ni kutoa unafuu katika bei
za chakula cha mifugo na kuhamasisha ufugaji.
x) Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10
badala ya asilimia 25 kwenye mabasi yenye uwezo wa
112
kubeba abiria zaidi ya 25 yanayotambuliwa katika HS
Code 8702.10.99 na HS Code 8702.90.99.
xi) Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10
badala ya asilimia 25 kwenye magari ya mizigo yenye
uwezo kati ya tani 5 na tani 20 yanayotambuliwa
katika HS Code 8704.22.90 kwa muda wa mwaka
mmoja.
xii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye magari ya mizigo yenye uwezo zaidi ya tani 20
yanayotambuliwa katika HS Code 8704.23.90 kwa
muda wa mwaka mmoja.
xiii) Kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya
asilimia 25 kwenye mabasi yatakayoagizwa kwa ajili ya
mradi wa mabasi wa jiji la Dar es Salaam
yanayotambuliwa katika HS Code 8702.10.99 na HS
Code 8702.90.99 kwa muda wa mwaka mmoja.
113
(xiv) Kutenganisha bidhaa zinazotambulika katika HS Code
8703.90.10 ili kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye pikipiki maalumu za kubeba wagonjwa
(motorcycle ambulances). Hatua hii inalenga
kuimarisha utoaji wa huduma ya kusafirisha wagonjwa
hasa katika maeneo ya vijijini.
xv) Kutenganisha virutubisho vya chakula
vinavyotambulika katika HS Code 2106.90.90 ili kutoza
ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia
25 kwenye virutubisho vya vyakula vya binadamu
(food supplements) ili kuendana na Sera ya Serikali ya
kuboresha afya za wananchi.
xvi) Kutenganisha bidhaa zinazotambulika katika HS Code
9616.10.00 ili kutoza ushuru wa forodha wa asilimia
10 badala ya asilimia 25 kwenye malighafi za
114
kutengeneza vifaa vya kunyunyizia (scent sprays and
other similar toilet sprays and mounts and heads).
(xvii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye matrekta ya kukokota mizigo
yanayotambuliwa katika HS Code 8701.20.90 kwa
muda wa mwaka mmoja. Hatua hii inalenga katika
kuboresha usafirishaji mizigo na kuongeza ufanisi
katika Sekta ya usafirishaji.
(xviii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye migahawa ya Majeshi ya Ulinzi kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
89. Mheshimiwa Spika, Mawaziri wa Fedha walikubaliana
kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kama
ifuatavyo:-
115
i) Kufanya marekebisho katika kifungu cha pili (2) cha Jedwali la
Tano la Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili
kuliwezesha Jeshi la Polisi kunufaika na msamaha wa ushuru wa
forodha kama linavyonufaika Jeshi la Ulinzi. Hatua hii inalenga
katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
ii) Kufanya marekebisho katika Jedwali la Tano (5) la Sheria ya
Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa nia ya kutekeleza
yafuatayo:
a) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye mitego
ya mbung’o (tsetse fly traps). Hatua hii inalenga katika
kuchochea ukuaji wa kilimo na kuboresha mazingira ya
kuvutia utalii hapa nchini.
b) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vifaa vya
kudhibiti usalama (security equipments: - hand held
metal detectors, walk through metal detectors, CCTV
cameras, bomb detectors and undercarriage mirrors).
116
Hatua hii inalenga katika kuboresha usalama wa raia na
mali zao.
c) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye magari
yanayoendeshwa kwa kutumia beteri (battery operated
vehicles/Golf carts). Hatua hii itaimarisha huduma za
kitalii na huduma za afya kwani magari haya yanaweza
kutumika kubeba wagonjwa ndani ya hospitali na kubeba
wageni na mizigo katika maeneo ya hoteli.
d) Kutoa msamaha wa Ushuru wa forodha kwenye magari
yanayotumika kubeba abiria katika viwanja vya ndege
(Apron buses) ili kuboresha huduma kwa wasafiri na
kuweka mazingira yenye kuvutia wageni na hasa watalii.
e) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi
za kutengeneza vifaa vinavyotumia mionzi ya jua (inputs
for manufacture of solar panels) kwa lengo la
kuhamasisha uzalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini.
117
f) Kupunguza kiwango cha ada ya ukaguzi (Destination
Inspection Fee) kinachotozwa kwenye bidhaa za biashara
zinazotoka nje kutoka asilimia 1.2 ya thamani ya huduma
ya kuzifikisha hadi bandarini (FOB) na kuwa asilimia 0.6.
Hatua hii inalenga katika kupunguza muda wa kuondoa
mizigo bandarini na kupunguza gharama za uingizaji
bidhaa na hivyo kupunguza bei za bidhaa kutoka nje.
Hatua hizi kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 4,669.7
M. Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi
90. Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kodi zinazopendekezwa
zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2011, isipokuwa pale
ilipoelezwa vinginevyo.
118
MFUMO WA BAJETI KWA MWAKA 2011/12:
91. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi
pamoja na misingi na sera za bajeti, SURAya Bajeti
inaonesha kwamba jumla ya shilingi bilioni 13,525.9
zinahitajika kutumika katika kipindi cha 2011/12. Jumla ya
mapato yanayotarajiwa ni shilingi bilioni 13,525.9. Kati ya
mapato hayo, Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi na
yasiyo ya kodi ya jumla ya shilingi bilioni 6,775.9, sawa na
asilimia 17.2 ya Pato la Taifa. Aidha, mapato kutoka vyanzo
vya Halmashauri ni shilingi bilioni 350.5. Kadhalika, Serikali
inategemea kukopa kiasi cha shilingi bilioni 2,475.9 kutoka
vyanzo vya ndani na nje. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni
810.9 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za
119
Serikali zinazoiva, shilingi bilioni 393.4 ni mikopo kutokana
na mauzo ya hatifungani za Serikali na shilingi bilioni 1,271.6
zitatokana na mikopo yenye masharti ya kibiashara.
92. Mheshimiwa Spika, washirika wa Maendeleo
wanatarajiwa kuendelea kuchangia bajeti kupitia misaada na
mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 3,923.6. Kati ya fedha
hizo, shilingi bilioni 869.4 ni misaada na mikopo ya kibajeti
na shilingi bilioni 3,054.1 ni misaada na mikopo kwa ajili ya
miradi ya maendeleo, ikijumuisha mifuko ya kisekta.
93. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, katika
mwaka 2011/12 Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi
bilioni 13,525.9 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.
Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 8,600.3
120
kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha
shilingi bilioni 3,270.3 kwa ajili ya mishahara ya watumishi
wa Serikali, taasisi na wakala za Serikali na shilingi bilioni
1,910.4 kwa ajili ya Mfuko Mkuu wa Serikali. Aidha, jumla ya
shilingi bilioni 4,925.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya
maendeleo, ambapo shilingi bilioni 1,871.5 ni fedha za ndani
na shilingi bilioni 3,054.1 ni fedha za nje.
94. Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya mfumo
wa Bajeti yaliyotolewa hapo juu, Sura ya Bajeti kwa mwaka
2011/12 itakuwa kama ifuatavyo:
121
Mapato Shilingi milioni
A: Mapato ya Ndani 6,775,952
(i) Mapato ya Kodi (TRA) 6,228,836
(ii) Mapato Yasiyo ya Kodi 547,116
B: Mapato ya Halmashauri 350,496
C: Mikopo na Misaada ya Nje 3,923,551
D: Mikopo ya Ndani 1,204,262
E: Mikopo ya Masharti ya Kibiashara 1,271,634
JUMLA YA MAPATO YOTE 13,525,895
F: Matumizi ya Kawaida 8,600,287
(i) Mfuko Mkuu wa Serikali 1,910,376
(ii) Mishahara 3,270,292
(iii)Matumizi Mengineyo 3,419,619
Wizara 2,727,472
Mikoa 49,981
Halmashauri 642,166
G: Matumizi ya Maendeleo 4,924,608
(i) Fedha za Ndani 1,871,471
(ii)Fedha za Nje 3,054,137
JUMLA YA MATUMIZI YOTE 13,525,895
122
HITIMISHO:
95. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2011/12 ni
mwendelezo wa juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo
wananchi. Bajeti hii imezingatia:
i) Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025;
ii) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini
Awamu ya Pili (MKUKUTA II);
iii) Malengo ya Maendeleo ya Milenia 2015;
iv) Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015;
v) Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania (MPAMITA);
vi) Mkakati wa Taifa wa Madeni; na
vii) Sera za Kijumla za Uchumi kwa mwaka 2011/12.
96. Mheshimiwa Spika, ili kufikia malengo hayo mapema
zaidi, kila mwananchi anapaswa kujituma na kushiriki kikamilifu,
123
kwa kutumia fursa zilizopo za kuzalisha mali na kujiongezea
kipato. Ni matumaini yangu kuwa utekelezaji sahihi wa Bajeti hii
utaiwezesha Serikali kuwaletea wananchi maendeleo
tunayokusudia. Bajeti ya mwaka 2011/12 imeandaliwa katika
kipindi ambacho nchi yetu inakabiliwa na changamoto ya
kiuchumi ikiwemo upungufu wa umeme na ongezeko la bei za
mafuta katika soko la dunia. Hali hii imetishia ustawi wa uchumi
na uwezo wa kukusanya mapato ya ndani. Serikali imejipanga
kukabiliana na changamoto hizi, ikiwa ni pamoja na kuharakisha
miradi ya uzalishaji umeme na uanzishwaji wa hifadhi kubwa ya
mafuta yanayoagizwa. Wakati Serikali ikichukua hatua hizi,
wananchi wanaombwa kuanza kutumia kwa uangalifu vyanzo
hivyo vya nishati, ili kupunguza gharama. Hivyo, ni matumaini ya
Serikali kwamba bajeti ya mwaka 2011/12 itatekelezwa kama
ilivyopangwa.
124
97. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Nne,
imedhamiria kwa dhati kuendeleza misingi imara ya kujenga
uwezo katika kukusanya mapato ya ndani. Hili litawezekana kwa
kuwekeza katika vichocheo vya ukuaji uchumi ili kuongeza wigo
wa mapato ya ndani kwa lengo la kutuongezea uwezo wa
kujitegemea. Kama nilivyoeleza hapo awali, maeneo yafuatayo
ya kimkakati yatazingatiwa katika mgao wa rasilimali katika
muda wa kati: nishati ya umeme; reli, bandari; TEHAMA; maji;
kilimo na kulinda mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu
na afya. Hivyo basi, hatuna budi kila mmoja wetu na kwa
pamoja kuongeza ubunifu katika uzalishaji wenye tija
utakaoongeza Pato la Taifa na hatimaye kuondokana na
umaskini.
125
98. Mheshimiwa Spika, bajeti hii imezingatia ushauri wa
Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Fedha na Uchumi na
Kamati nyingine za Kisekta. Pia, imezingatia mawazo na
mapendekezo ya wadau mbalimbali, wakiwemo
wafanyabiashara, wenye viwanda, sekta ya kilimo, utalii na
wengine wengi. Nawashukuru wote hao kwa mawazo na ushauri
wao.
99. Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kuwashukuru
wapiga kura wangu wote wa Jimbo la Kilosa kwa kunichagua
tena kuwa Mbunge wao kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Napenda kuwaahidi kwamba tutashirikiana pamoja kuliletea
maendeleo Jimbo letu la Kilosa. Ninaamini kwamba
sitawaangusha. Mwisho nachukua pia nafasi hii kumshukuru
kipekee mke wangu mpendwa kwa kuwa msaada mkubwa
kwangu.
126
100. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza awali Serikali
inatambua makali ya maisha yanayowakabili wananchi. Kuna tatizo la
upungufu wa umeme, kuongezeka kwa bei za mafuta ya petroli na
gharama za usafiri, tatizo la ajira na haja ya kuboresha hifadhi
yetu ya chakula. Serikali sikivu ya Chama cha Mapinduzi
imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto hizo. Ni
matumaini ya Serikali kwamba hatua za kukabiliana na
changamoto hizo nilizozieleza zitasaidia kuondoa kero hizo na
hivyo kuboresha maisha ya wananchi.
101. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
No comments:
Post a Comment